• HABARI MPYA

  Jumanne, Julai 28, 2015

  ARTURO VIDAL AANGUKA MIAKA MINNE BAYERN MUNICH

  KIUNGO wa kimataifa wa Chile, Arturo Vidal amekamilisha uhamisho wa Pauni Milioni 28 kwenda Bayern Munich ya Ujerumani kutoka Juventus ya Italia na kusema usajili huo ni kutimia kwa ndoto zake.
  Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 amesaini Mkataba wa miaka minne leo baada ya kufuzu vipimo vya afya mjini Munich jana.
  Taarifa katika tovuti ya klabu hiyo imesema kwamba; "Jumanne majira ya mchana, Arturo Vidal amesaini Mkataba wa miaka minne na FC Bayern, ambao utamuweka hapa Munich hadi mwaka 2019. 
  Arturi Vidal akikabidhiwa jezi namba 23 na Rais wa Bayern Munich, Karl-Heinz Rummenigge leo baada ya kusaini leo PICHA ZAIDI GONGA HAPA
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: ARTURO VIDAL AANGUKA MIAKA MINNE BAYERN MUNICH Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top