• HABARI MPYA

  Jumanne, Julai 21, 2015

  AZAM FC YAENDELEA KUNG’ARA KOMBE LA KAGAME, YAWAPIGA WASUDAN 2-0 TAIFA

  Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
  AZAM FC imeendeleza wimbi la ushindi katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame baada ya jioni ya leo kuifunga Malakia ya Sudan Kusini mabao 2-0 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Katika mchezo huo wa Kundi C, hadi mapumziko, Azam FC walikuwa mbele kwa bao 1-0 lililofungwa na Nahodha wake, John Raphael Bocco ‘Adebayor’.
  Bocco alifunga bao hilo dakika ya 26 baada ya kuanzishiwa mpira wa adhabu na beki Aggrey Morris Ambroce. 
  Kipindi cha pili, Azam FC inayofundishwa na Muingereza Stewart John Hall ilifanya mabadiliko ya tija na kufanikiwa kuunenepesha ushindi wao.
  Mshambuliaji kutoka Ivory Coast, Kipre Herman Tchetche aliyeingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Ame Ali, aliifungia Azam FC bao la pili dakika ya 51 akimalizia pasi ya beki Shomary Kapombe.
  John Bocco kushoto akipongezwa na Frank Domayo na Aggrey Morris nyuma baada ya kufunga bao la kwanza

  Azam FC sasa inafikisha pointi sita baada ya mechi mbili na kujiweka katika mazingira mazuri ya kwenda Robo Fainali.
  Katika mchezo uliotangulia, Al Shandy ya Sudan ilitoka sare ya kufungana mabao 2-2 na LLB FC ya Sudan.
  Kikosi cha Azam FC kilikuwa; Manula Aishi Salum, Shomari Kapombe, Gadiel Michael/Farid Mussa dk46, Abdallah Kheri, Pascal Wawa, Agrey Morris Ambros, Jean Mugiraneza, Salum Abubakar ‘Sure Boy’/Mudathir Yahya dk64, Frank Domayo, John Bocco na Ame Ali/Kipre Tchetche dk46. 
  Malakia; Kennedy Santolino, David Dada Stephen, Makir Albino Mior, Lubari Zeriba Ibrahim, Wisely Onguso Arasa, Saddam Opera Peter, Samuel Sskamatte, Mahmoud Al Taher/Gabriel John dk72, Ahmed Sani, Soh koodjou Mfomo/Gassim Lado dk84 na Yengo Son Ngum.
  Mshambuliaji wa Azam FC, Ame Ali akimtoka beki wa Malakia, David Dada Stephen jioni ya leo Taifa
  Mshambuliaji wa Azam FC, John Bocco akimtoka beki wa Malakia, Wisely Onguso Arasa jioni ya leo Taifa
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: AZAM FC YAENDELEA KUNG’ARA KOMBE LA KAGAME, YAWAPIGA WASUDAN 2-0 TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top