• HABARI MPYA

  Alhamisi, Julai 30, 2015

  IBRAHIMOVIC AWAADHIBU MAN UNITED WALALA 2-0 KWA PSG MAREKANI

  MANCHESTER United imepoteza mechi ya kwanza katika ziara ya kujiandaa na msimu nchini Marekani, baada ya kufungwa mabao 2-0 na PSG usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Soldier Field mjini Chicago.
  Blaise Matuidi aliifungia PSG bao la kwanza dakika ya 25 akimtungua vizuri kipa David de Gea anayetakiwa na Real Madrid, kabla ya Zlatan Ibrahimovic kufunga la pili akimalizia pasi ya Maxwell. 
  De Gea hakuwa katika ubora wake na kocha Louis van Gaal akamtoa kipindi cha pili, wakati wachezaji wapya Memphis Depay, Bastian Schweinsteiger, Morgan Schneiderlin na Matteo Darmian wote walicheza.
  United sasa inarejea nyumbani tayari kwa mchezo wa ufunguzi wa Ligi Kuu England dhidi ya Tottenham Jumamosi ya Agosti 8. 
  Kikosi cha Manchester United kilikuwa; De Gea/Johnstone dk45, Darmian, Jones/Smalling dk65, Blind, Shaw/Valencia dk65, Carrick/Goss dk81, Schweinsteiger/Schneiderlin dk45, Mata/Lingard dk81, Memphis, Young/Pereira dk45 na Rooney.
  PSG; Trapp, Maxwell/Digne dk45, Silva/Sabaly dk67, Aurier/Luiz dk45, Van der Wiel/Marquinhos dk45, Matuidi/Kimpembe dk73, Stambouli/Nkunku dk73, Verratti/Rabiot dk67, Moura/Ongenda dk73, Augustin/Cavani dk45 na Ibrahimovic/Bahebeck dk70.
  Zlatan Ibrahimovic akishangilia baada ya kuifungia bao PSG dhidi ya Man United usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Soldier Field mjini Chicago PICHA ZAIDI GONGA HAPA
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: IBRAHIMOVIC AWAADHIBU MAN UNITED WALALA 2-0 KWA PSG MAREKANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top