• HABARI MPYA

  Jumatano, Julai 29, 2015

  CHELSEA YAIBWAGA BARCA KWA MATUTA BAADA YA SARE YA 2-2 MAREKANI

  CHELSEA imeifunga Barcelona kwa penalti 4-2 baada ya sare ya 2-2 katika mchezo wa kirafiki wa kujiandaa msimu Uwanja wa FedEx Field, mjini Washington, Marekani usiku wa kuamkia leo mbele ya mashabiki 78,000.
  Eden Hazard aliipasua ngome ya Barcelona na kuifungia Chelsea bao la kwanza dakika ya 10, kabla ya Luis Suarez kuisawazishia Barca dakika ya 52.
  Refa akamchanganya Kurt Zouma wakati anajaribu kuokoa mpira uliopigwa na Sandro na ukatinga nyavuni kuipatia Barcekona bao la pili dakika ya 66, lakini bahati nzuri kwao, Gary Cahill akaisawazishia Chelsea akiwa anatoka damu puani dakika ya 86.
  Mshambuliaji aliyehamia Chelsea kutoka Manchester United alikokuwa anacheza kwa mkopo, Radamel Falcao akafunga penalti ya kwanza ya The Blues mwishowe timu ya Jose Mourinho ikaifunga Barcelona 4-2 kwa matuta.
  Penalti nyingine za Chelsea zilifungwa na Moses, Ramires na Loic Remy wakati za Barcelona Iniesta alifunga, Halilovic iligonga mwamba wa juu, ya Pique iliokolewa na kipa wa Chelsea, Thibaut Courtois, Sandro alifunga.
  Kikosi cha Chelsea kilikuwa: Courtois, Ivanovic, Zouma, Cahill/Chalobah dk87, Azpilicueta/Terry dk59, Fabregas/Moses dk64, Matic/Mikel dk61, Kenedy/Willian dk46, Oscar/Ramires dk46, Hazard/Falcao dk68 na Costa/Remy dk60.
  Barcelona: Ter Stegen (Masip 60), Douglas/Roberto dk17, Bartra/Pique dk59, Mathieu/Vermaelen dk59, Adriano/Alba dk59, Rakitic/Iniesta dk60, Busquets/Rafinha dk61, Suarez/Pedro dk62, Munir/Halilovic dk73, Sandro, Gumbau/Samper dk61.
  Radamel Falcao akibinuka tik tak katika mchezo huo PICHA ZAIDI GONGA HAPA
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: CHELSEA YAIBWAGA BARCA KWA MATUTA BAADA YA SARE YA 2-2 MAREKANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top