• HABARI MPYA

  Ijumaa, Julai 24, 2015

  RONALDO, BENZEMA WOTE WAFUNGA REAL MADRID IKIITANDIKA MAN CITY 4-1

  TIMU ya Real Madrid imeiadhibu vikali Manchester City baada ya kuifunga mabao 4-1 katika mchezo wa Kombe la Mabingw awa Kimataifa kwenye Uwanja wa Kriketi mjini Melbourne.
  Mabao ya Real yamefungwa na Karim Benzema dakika ya 21, Cristiano Ronaldo dakika ya 25, Pepe dakika ya 44 na Denis Cheryshev dakika ya 73, wakati bao pekee la Man City limefungwa na Yaya Toure kwa penalti dakika ya 45 na ushei.
  Penalti hiyo ilitolewa baada ya beki wa Real, Sergio Ramos kuunawa mpira.
  KIkosi cha Real Madrid kilikuwa: Navas, Carvajal, Pepe, Ramos, Marcelo, Kroos, Modric, Isco, Bale, Ronaldo na Benzema.Manchester City: Hart, Sagna, Denayer, Humphreys, Kolarov, Toure, Fernando, Delph, Nasri, Silva na Sterling.
  Cristiano Ronaldo akishangilia baada ya kuifungia Real Madrid dhidi ya Manchester City leo PICHA ZAIDI GONGA HAPA
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: RONALDO, BENZEMA WOTE WAFUNGA REAL MADRID IKIITANDIKA MAN CITY 4-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top