• HABARI MPYA

  Jumapili, Julai 26, 2015

  MECHI YA YANGA NA AZAM FC YANUKIA ROBO FAINALI KAGAME 2015, ITAKUWA JUMATANO

  Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
  MECHI ya mahasimu wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Azam FC na Yanga SC inanukia katika Robo Fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki, Kombe la Kagame mapema wiki ijayo.
  Yanga SC leo wanacheza mechi yao ya mwisho ya Kundi A Kombe la Kagame dhidi ya Khartoum N ya Sudan Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia Saa 10:00 jioni.
  Mchezo huo utatanguliwa na mechi nyingine ya kundi hilo kati ya Gor Mahia ya Kenya na Telecom ya Djibouti.
  KMKM ya Zanzibar imemaliza mechi zake za kundi hilo na imekwisharejea Zanzibar baada ya kutolewa kufuatia kuambulia pointi tatu za ushindi wa mechi moja dhidi ya vibonde, Telecom 1-0.

  Mshambuliaji wa Yanga SC, Kpah Sherman (kushoto) akiwania mpira dhidi ya beki wa Azam FC, Shomary Kapombe katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu huu. Je, timu hizo zitakutana Robo Fainali Kombe la Kagame?

  Telecom wamefungwa na kila timu katika kundi hilo na leo wanacheza mechi yao ya mwisho dhidi ya Gor kuanzia Saa 8:00 mchana.
  Khartoum N na Gor Mahia zote zina pointi saba kila moja baada ya kushinda mechi mbili mbili na kutoa sare moja katika mechi baina yao, wakati Yanga SC ni ya tatu kwa pointi zake sita za ushindi wa mechi mbili.
  Mshindi wa kwanza wa Kundi A atakutana na Malakia ya Sudan Kusini katika Robo Fainali, mshindi wa pili atakutana na Azam FC wakati mshindi wa tatu atakutana na APR ya Rwanda.
  Ikiwa sasa inashika nafasi ya tatu, Yanga SC ikifanikiwa kuifunga Khartoum N leo, inaweza ikapanda kileleni iwapo, Telecom watamudu hata kulazimisha sare na Gor Mahia, jambo ambalo halitarajiwi. Matarajio ni Gor kushinda, tena ushindi mnono.
  Na Yanga SC kuifunga Khartoum N si jambo jepesi pia, kwani timu hiyo inayofundishwa na Mghana Kwesi Appiah imeonyesha ubora wa soka yake katika mechi zilizotangulia.
  Yanga SC ikiongoza kundi, itacheza na Malakia, ikiwa ya pili itacheza na Azam FC na ikiwa ya tatu itakutana na APR, je itaangukia wapi?
  Dakika 180 za mechi mbili za leo (Gor Mahia Vs Telecom na Yanga SC Vs Khartoum N) ndiyo zitatoa majibu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam- ila mechi ya Yanga na Azam FC inanukia Robo Kagame 2015. 
  Mshambuliaji hatari wa Azam FC, Kipre Tchetche jana amefunga mabao mawili katika ushindi wa 5-0 dhidi ya Adama City

  Donald Ngoma amekuwa tishio kwa mabeki wa timu pinzani Kombe la Kagame akiwa na Yanga SC 

  MISIMAMO YA MAKUNDI KOMBE LA KAGAME

  Kundi A  PWDLGFGAGDPts
  1Khartoum (Sudan)32107167
  2Gor Mahia (Kenya)32106337
  3Yanga (Tanzania)32016246
  4Telecom (Djibouti)300329-90

  Kundi B  PWDLGFGAGDPts
  1APR (Rwanda)33005149
  2Al Shandy (Sudan)31115504
  3LLB (Burundi)302134-12
  4Heegan (Somalia)301225-3
  1

  Kundi C  PWDLGFGAGDPts
  1Azam (Tanzania)33008089
  2KCCA (Uganda)32012116
  3Malakia (S. Kusini)310224-23
  4Adama (Ethiopia)300318-70  Ratiba ya Kombe la Kagame

  Jumanne Julai 28, 2015
  APR vYanga/Gor/KhartoumSaa 8:00 Mchana
  Yanga/Gor/Khartoum
  vMalakiaSaa 10:00 Jioni
  Jumatano Julai 29, 2015


  Al ShandyvKCCASaa 8:00 Mchana
  Azam FCv
  Yanga/Gor/Khartoum
  10:00 Jioni

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MECHI YA YANGA NA AZAM FC YANUKIA ROBO FAINALI KAGAME 2015, ITAKUWA JUMATANO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top