• HABARI MPYA

  Jumanne, Julai 21, 2015

  COASTAL UNION YASAJILI 13 WAPYA TAYARI KWA MSIMU MPYA LIGI KUU

  Na Mwandishi Wetu, TANGA
  KLABU ya Coastal Union imeweza kusajili wachezaji 13 wakiwemo kipa Jackson Sabweto kutoka SC Villa ya Uganda aliyesaini mkataba wa miaka miwili na Yossouph Sabo kutoka Younde FC ya Cameroon aliyesaini mwaka mmoja, ambao wataitumikia timu hiyo katika michuano ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu ujao.
  Akizungumza na waandishi wa habari jana,Ofisa Habari wa Coastal Union,Oscar Assenga amesema kuwa wachezaji ambao wamesajiliwa wametoka timu mbalimbali hapa nchini na nje ya nchi.
  Aliwataja wachezaji hao kuwa ni Abasalim Chidebele ambaye ni mshambuliaji kutoka timu ya Stand United, Kiungo Mkabaji Adeyum Salehe kutoka JKU ya Zanzibar,Kiungo Mshambuliaji Nasoro Kapama kutoka Ndanda FC ya Mtwara,Beki wa kati Ernest Mwalupani kutoka Ndanda FC ya Mtwara.

  Wengine ni Beki wa Kushoto ,Yassin Mustapa Salim kutoka Stand United,Kiungo Sultan Juma kutoka klabu ya African Sports,Mshambuliaji Ahmde Shiboli kutoka Klabu ya African Sports,Mohamed Hamis Mititi ambaye ni mchezaji huru.
  Assenga amewataja wachezaji wengine kuwa ni Benedict Haule ambaye alisajiliwa akiwa kama mchezaji huru ambaye ni mlinda mlango,Mshambuliaji Ismail  Mohamed Suma kutoka Stand United, winga wa kushoto ambaye ni mchezaji huyo Patrick Protas Kamuhagile.
  Wachezaji wa zamani waliobaki kutimukia klabu hiyo kuwa ni Bakari Mbwana “Kibacha”,Abdallah Mfuko,Hamadi Juma,Ibrahim Chuma,Ike Bright Obina,Abdulhalim Humud,Godfrey Wambura,Ayoub Semtawa na Sued Tumba.
  Wakati huo huo wachezaji uongozi wa Coastal Union umewapandisha wachezaji watano kutoka timu ya vijana ya Coastal Union kutokana na uwezo wao kuwa mzuri na wa kuridhisha.
  Waliopandishwa ni Mohamed Shekuwe,Sabri Sabri,Tumaini Bakari,Fikirini Suleiman na mtenje Albano
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: COASTAL UNION YASAJILI 13 WAPYA TAYARI KWA MSIMU MPYA LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top