• HABARI MPYA

    Sunday, July 19, 2015

    YANGA SC YAWATEMA JAVU, ZAHIR NA KIPA MPYA KIKOSI CHA KAGAME

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    YANGA SC haijawajumuisha Mudathir Khamis, Rajab Zahir, Edward Charles na Hussein Javu katika kikosi chake cha wachezaji 20, kwa ajili ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame iliyoanza jana Dar es Salaam.
    Kipa Mudathir amesajiliwa kutoka KMKM ya Zanzibar, wakati Zahir, Charles na Javu walikuwepo kwenye kikosi cha Yanga SC msimu uliopita.
    Yanga SC ilianza vibaya kwa kufungwa mabao 2-1 na Gor Mahia ya Kenya katika mchezo wa ufunguzi wa Kundi A Uwanja wa Taifa, Dar e Salaam. 
    Yanga SC ilianza vibaya kwa kufungwa 2-1 na Gor Mahia jana

    Na makocha wa timu hiyo, Mholanzi, Hans van der Pluijm na mzalendo Charles Boniface Mkwasa wamewaacha Zahir, Charles na Javu katika kikosi cha Kagame.
    Majina ambayo Yanga SC imewasilisha Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) kwa ajili ya Kagame ya 2015 ni makipa; Ally Mustafa na Deo Munishi ‘Dida’.
    Mabeki ni Nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Juma Abdul, Kevin Yondani, Joseph Zutah, Oscar Joshua, Mwinyi Haji na Pato Ngonyani.
    Viungo ni Mbuyu Twite, Simon Msuva, Andrey Coutinho, Haruna Niyonzima, Salum Telela, Deus Kaseke na Godfrey Mwashiuwa, wakati washambuliaji ni Amisi Tambwe, Kpah Sherman, Malimi Busungu na Donald Ngoma.
    Yanga SC itashuka tena dimbani Jumatano kumenyana na Telecom ya Djibouti Saa 10: 00 jioni mchezo ambao utatanguliwa na mechi kati ya Khartoum na KMKM na KCCA na Adama City.
    John Bocco (kushoto) akiwania mpira dhidi ya mabeki wa KCCA
    Mshambuliaji Mtanzania wa KCCA, Shaaban Kondo (kushoto) akipambana na beki wa Azam FC, Serge Wawa Pascal
    Beki wa Azam FC, Erasto Nyoni (kulia) akimtoka beki wa KCCA, Hakim Senkumba
    Kiungo wa Azam FC, Salum Abubakar 'Sure Boy', Hakim Sekumba
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA SC YAWATEMA JAVU, ZAHIR NA KIPA MPYA KIKOSI CHA KAGAME Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top