• HABARI MPYA

    Sunday, July 26, 2015

    YANGA SC KUIVAA AZAM FC JUMATANO ROBO FAINALI KAGAME, NI BAADA YA KUWACHAPA WASUDAN 1-0 TAIFA LEO

    Amisi Tambwe akikimbia kushangilia baada ya kuifungia bao pekee Yanga SC dhidi ya Khartoum N ya Sudan leo

    RATIBA YA ROBO FAINALI KAGAME 2015   

    Jumanne Julai 28, 2015
    APR Vs Khartoum N (Saa 8:00 mchana)
    Gor Mahia Vs Malakia (Saa 10:00 jioni)
    Julai 29, 2015
    Al Shandy Vs KCCA (Saa 8:00 mchana)
    Azam FC Vs Yanga SC (Saa 10:00 jioni)
    Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
    YANGA SC itamenyana na Azam FC katika Robo Fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame Jumatano Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Hiyo inafuatia ushindi wa bao 1-0 jioni ya leo dhidi ya Khartoum N ya Sudan katika mchezo wa mwisho wa Kundi A Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Na kwa matokeo hayo, Yanga SC inamaliza katika nafasi ya pili kwenye kundi hilo kwa pointi zake tisa, baada ya kushinda mechi tatu, zikiwemo dhidi ya KMKM ya Zanzibar 2-0 na Telecom ya Djibouti 3-0.
    Bao hilo pekee la Yanga SC leo limefungwa na mshambuliaji wake wa kimataifa wa Burundi, Amisi Joselyn Tambwe dakika ya 30 akimalizia kwa kichwa kona iliyochongwa na Nahodha Haruna Niyonzima kutoka Rwanda dakika ya 30.
    Sifa za kipekee zimuendee kipa Ally Mustafa ‘Barthez’ aliyeokoa michomo mingi ya hatari langoni mwake hadi Yanga SC kuulinda ushindi huo. 
    Safu ya ulinzi ya Khartoum yenye mabeki warefu ilikuwa kikwazo cha mashambulizi ya mipira mirefu kutoka pembeni ya Yanga, kwani waliicheza kwa wingi na kuiondosha katika hatari.
    Yanga SC inamaliza katika nafasi ya pili nyuma ya Gor Mahia ya Kenya yenye pointi 10, wakati Khartoum kwa pointi zake saba inamaliza nafasi ya tatu, ingawa nayo imefuzu Robo Fainali.
    Winga wa Yanga SC, Simon Msuva akienda chini baada ya kukwatuliwa na beki wa Khartoum N, Antony Akumu Agay leo. Kulia ni Ahmed Adam.
    Mfungaji wa bao pekee la Yanga SC, Amisi Tambwe akiwatoka mabeki wa Khartoum N
    Beki wa Yanga SC, Joseph Zuttah akimtoka beki wa Khartoum, Wagdi Awad
    Mshambuliaji wa Yanga SC, Malimi Busungu akimtoka beki wa Kahrtoum N, Ahmad Adam

    Winga Mbrazil wa Yanga SC, Andrey Coutinho akimtoka beki wa Khartoum N, Domenic Abui

    Robo Fainali za kwanza zinatarajiwa kuchezwa Jumanne kati ya APR ya Rwanda na Khartoum N na Gor Mahia na Malakia ya Sudan Kusini, wakati za pili zitachezwa Jumatano kati ya Al Shandy ya Sudan na KCCA ya Uganda na baadaye, Yanga SC na Azam FC zote za Dar es Salaam.
    Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Ally Mustafa, Jopseph Zutah, Oscar Joshua/Mwinyi Hajji Mngwali dk46, Pato Ngonyani, Kevin Yondani/Nadir Haroub ‘Cannavro’ dk83, Mbuyu Twite, Simon Msuva, Haruna Nyonzima, Amisi Tambwe, Malimi Busungu na Andrew Coutinho/Godfrey Mwashiuya dk65.
    Khartoum N; Mohamed Ibrahim, Amin Ibrahim, Hamza Daoud, Salaheldin Mahamoud, Samawal Merghani, Wagdi Awad, Antony Akumu Agay, Domenic Abui, Atif Khalif/Ismail Baba dk46, Badreldin Eldoon/Marwan Salah dk62 na 
    Ahmed Adam.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA SC KUIVAA AZAM FC JUMATANO ROBO FAINALI KAGAME, NI BAADA YA KUWACHAPA WASUDAN 1-0 TAIFA LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top