• HABARI MPYA

  Jumatatu, Julai 27, 2015

  BEKI WA SIMBA SC ANG’ARA ULAYA, APIGA BAO TIMU YAKE IKISHINDA 5-0 KOMBE LA UJERUMANI

  Emily Mugeta (jezi nyekundu) akiichezea NSU jana katika Kombe la Wurttemberg
  TIMU ya Neckarsulm Sports Union (NSU), yenye Mtanzania Emily Mugeta, imetinga Raundi ya pili ya Kombe la Wurttemberg baada ya kuichapa mabao 5-0 Spvgg Groningen-Satteldorf jana. 
  Kombe la Wurttemberg ni moja ya mashindano 21 ya mikoa katika soka ya Ujerumani, ambayo bingwa wake huingia Raundi ya Kwanza ya Kombe la Ujerumani, linaloshirikisha timu zote za nchi hiyo.
  Mabao ya NSU yalifungwa na wachezaji wapya wa timu hiyo ya Daraja la Tano, Mtanzania Emily Mugeta dakika ya 17, Yannick Titzmann matatu dakika za 19, 27 na 34 na Philipp Seybold dakika ya 52. Mabao mawili yalitokana na krosi za Mugeta.
  Baada ya mchezo huo, kocha wa NSU, Thorsten Damm  alisema; “Leo nilikuwa katika mazingira mazuri, tulikuwa vizuri na tulitawala mchezo tangu kipindi cha kwanza, nawapongeza vijana wanfu,”.
  Akizungumza na BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE kwa simu kutoka Baden-Wurttemberg Neckarsulm mjini Heilbronn, Ujerumani, Mugeta amesema kwamba amefurahi kuwa na mwanzo mzuri katika klabu yake hiyo mpya.
  “Nimefurahi sana nimecheza kucheza hatua za awali za Kombe la Ujerumani katika timu yangu mpya na tumeshinda,”amesema mchezaji huyo wa zamani wa Simba SC. Katika Raundi ya Pili, NSU sasa itamenyana na TSV Schwaikheim wikiendi ijayo.
  Kikosi cha NSU kilikuwa: Susser, Schaaf, Kappes, Seybold/Marche dk62, Mugeta/Celiscak dk72, Busch, Neupert, Gotovac, Gerstle/Gorl dk72, Titzmann na Hess.
  Emily Mugeta wakati anasainishwa na kocha Thorsten Damm Mei mwaka huu
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: BEKI WA SIMBA SC ANG’ARA ULAYA, APIGA BAO TIMU YAKE IKISHINDA 5-0 KOMBE LA UJERUMANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top