Na Princess Aasia, DAR ES SALAAM
MABINGWA wa zamani wa Tanzania na Afrika Mashariki na Kati, Simba SC wameondoka Dar es Salaam asubuhi ya leo kwenda Lushoto mkoani Tanga kuweka kambi maalumu kwa ajili ya kujitayarisha na Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Washindi hao wa pili wa Kombe la CAF (sasa Shirikisho) mwaka 1993, wameondoka Saa 4:00 asubuhi na kikosi cha wachezaji 21 wakiambatana na benchi la ufundi la watu watano, likiongozwa na Kocha Mkuu Muingereza, Dylan Kerr.
Mshambuliaji Mganda, Emmanuel Okwi aliyeoa hivi karibuni hakuwemo kwenye msafara, wakati pia wachezaji wengine kutoka Burundi inaelezwa wataungana na wenzao huko wiki ijayo.
Wachezaji walioondoka ni makipa; Peter Manyika
David Robert Kisu, Denis Deonis Richard, mabeki, Hassan Ramadhani ‘Kessy’, Samih Hajji Nuhu, Murushid Juuko na Mohamed Fakih Khatib.
Viungo ni Awadh Juma, Simon Sserenkuma, Peter Mwalyanzi na washambuliaji Mussa Hassan Mgosi, Ibrahim Hajib, Hamisi Kizza, Elias Maguli, Issa Abdallah Ngoa, Emmanuel Alex Massawe, Michael Mgimwa, Mbaruku Yusuph na Saidi Issa.
Benchi la ufundi limeongozwa na kocha Mkuu, Dylan Kerr, Kocha Msaidizi, Suleiman Matola, Kocha wa makipa Iddi Salim Abdul, Kocha wa viungo, Dusan Momcilovic na Daktari Yassin Gembe.
Abdi Banda na Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ watafanyiwa vipimo kesho kabla ya kwenda kambini, wakati Jonas Mkude atawasubiri wachezaji waliokuwa Taifa Stars, Hassan Isihaka, Ramadhani Singano na Said Ndemla aungane nao.

![]() |
| Kikosi cha Simba SC kilichokwenda Lushoto leo |

.png)
0 comments:
Post a Comment