• HABARI MPYA

    Friday, July 03, 2015

    ANTHONY JOSHUA ULINGONI TENA SEPTEMBA 12 02 ARENA

    BONDIA Anthony Joshua anaweza kuzipiga na Gary Cornish kabla ya kuzichapa na mpinzani wake wa zamani katika ngumi za Ridhaa, Dillian Whyte baadaye mwaka huu.
    Mbabe huyo wa uzito wa juu, atarejea ulingoni ukumbi wa O2 Arena mjini London, baada ya ushindi wa Knockout (KO) raundi ya pili dhidi ya Kevin Johnson, Septemba 12.
    Hatapigana mjini Manchester Julai 18, Martin Murray amechukua nafasi yake na ndiyo kwanza amerejea kutoka mapumzikoni tayari kwa maandalizi ya pambano lijalo miezi miwili ijayo.
    Inafahamika kwamba Scot Cornish - akiwa na rekodi ya ushindi wa mapambano 21, kati ya hayo 12 kwa Knockout na yuko chini ya promota Kellie Maloney - atakuwa mpinzani wa baadaye wa Joshua. 
    Rekodi ya Joshua ya kutowavusha zaidi ya raundi ya tatu wapinzani wake wote katika mapambano yake 13 ya ngumi za wakati pia Cornish anataka kuwa Mscotland wa kwanza kutwaa ubingwa wa dunia wa uzito wa juu.
    Anthony Joshua aterejea ulingoni September 12 ukumbi wa O2 Arena mjini London
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ANTHONY JOSHUA ULINGONI TENA SEPTEMBA 12 02 ARENA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top