NAHODHA wa zamani wa Liverpool, Steven Gerrard alikuwa kivutio kikubwa leo wakati anatambulishwa katika klabu yake mpya, LA Galaxy ya Marekani.
Gwiji huyo wa Wekundu aliondoka Merseyside mwishoni mwa msimu, baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa maisha yake yote ya awali ya soka Anfield na kwenda kumalizia soka yake kwa mabingwa wa MLS, LA Galaxy.
Klabu hiyo ya Marekani imetoa picha ya kwanza rasmi ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 35 akiwa ameshika jezi namba nane (8), ikiambatanishwa na maelezo: 'Karibu Los Angeles, Steven Gerrard! #GR8NESS'.
Steven Gerrard akitabasamu wakati ameshika jezi ya timu yake mpya LA Galaxy mbele ya alama ya Hollywood
Kiungo huyo anatarajiwa kutambulishwa wakati wa mapumziko katika mchezo wa Jumamosi dhidi ya Toronto.
Baada ya hapo atavaa jezi ya Galaxy kwa mara ya kwanza katika mazoezi ya wazi Jumanne kuelekea Mkutano na Waandishi wa Habari huku mechi yake ya kwanza ikiwa ni Julai 17 nyumbani kwa San Jose Earthquakes.



.png)
0 comments:
Post a Comment