• HABARI MPYA

    Sunday, April 05, 2015

    YANGA SC WAINGIA KAMBINI KESHO KUJIANDAA NA COASTAL, MBEYA CITY

    Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
    YANGA SC inaingia kambini kesho Dar es Salaam kujiandaa na mchezo wake ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Coastal Union Jumatano, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Yanga SC imerejea jana usiku Dar es Sakaam ikitokea Zimbabwe ambako ilifanikiwa kutinga hatua ya 16 Bora michuano ya Kombe ka Shirikisho Afrika, licha ya kufungwa bao 1-0 na wenyeji FC, FC Platinum Uwanja wa Uwanja wa Mandava, Zvishavane nchini Zimbabwe.
    Kwa matokeo hayo, Yanga SC imesonga mbele kwa ushindi wa jumla wa mabao 5-2 baada ya awali kushinda mabao 5-1 mjini Dar es Salaam.
    Yanga SC walirejea usiku wa jana saa chache baada ya mechi yao na FC Platinum

    Katika mchezo wa jana, kipa Ally Mustafa Mtinge ‘Barthez’ ndiye aliyekuwa nyota  baada ya kuokoa hatari nyingi langoni mwake.
    Walter Musona ndiye aliyeifungia Platinum bao dakika ya 29 akimalizia pasi ya Ngoma aliyempiga chenga beki Juma Abdul upande wa kulia wa Uwanja.
    Yanga SC inaongoza Ligi Kuu kwa pointi zake 40, baada ya mechi 19, ikifuatiwa na mabingwa watetezi, Azam FC wenye pointi 36 za mechi 18. Yanga SC watashuka tena dimbani mwishoni mwa wiki kumenyana na Mbeya City Aprili 11.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA SC WAINGIA KAMBINI KESHO KUJIANDAA NA COASTAL, MBEYA CITY Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top