• HABARI MPYA

    Sunday, April 05, 2015

    TAIFA STARS KUANZA NA UGANDA KUFUZU CHAN, IKIFUZU HAPO ITAKUTANA NA SUDAN

    Na Mwandishi Wetu, CAIRO
    TANZANIA itaanza na Uganda katika mechi za kuwania kufuzu Fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) nchini Rwanda mwaka 2016, ambazo huhusisha wachezaji wanaocheza ligi za nchini mwao pekee.
    Mechi za kwanza zitachezwa kati ya Juni 19, 20 na 21 mwaka huu na marudiano yatakuwa kati ya Julai 3, 4 na 5 mwaka 2015.
    Kwa mujibu wa ratiba ya michuano hiyo iliyopangwa leo mjini Cairo, Misri iwapo Tanzania itaitoa Uganda, itamenyana na Sudan iliyofuzu moja kwa moja Raundi ya Kwanza.
    Hii ndiyo timu inayoandaliwa kucheza mechi za kufuzu CHAN

    Katika droo hiyo iliyoongozwa na Katibu wa CAF, Hicham El Amrani aliyesaidiwa na Makamu wa Pili wa Rais wa CAF, Almamy Kabele Camara, ambaye ni Rais wa Kamati ya Maandalizi ya CHAN, Kenya itaanza na Ethiopia na Burundi itacheza na Djibouti kwa kanda ya Afrika Mashariki na Kati.
    Mshindi kati ya Kenya na Ethiopia atakutana na mshindi kati ya Burundi na Djibouti katika Raundi ya Kwanza.
    Mechi za kwanza za hatua hiyo zitachezwa kati ya Oktoba 16, 17 na 18 na marudiano kati ya Oktoba 23, 24 na 25 mwaka huu na washindi wa mechi hizo za Raundi ya Kwanza watafuzu moja kwa moja kwenye fainali hizo, wakiungana na wenyeji Rwanda pamoja na nchi za kanda nyingine. Kwa Ratiba kamili gonga hapo> Click here for the fixtures
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TAIFA STARS KUANZA NA UGANDA KUFUZU CHAN, IKIFUZU HAPO ITAKUTANA NA SUDAN Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top