• HABARI MPYA

    Sunday, April 05, 2015

    SAMATTA AING’ARISHA MAZEMBE, YAENDA 16 BORA LIGI YA MABINGWA AFRIKA

    MTANZANIA Mbwana Ally Samatta (pichani juu) amefunga bao moja katika ushindi wa 3-1 dhidi ya Mamelodi Sundowns katika mchezo wa marudiano hatua ya 32 Bora Ligi ya Mabingwa Afrika Uwanja wa Mazembe, Lubumbashi.
    Matokeo hayo, yanaifanya Mazembe isonge hatua ya 16 Bora kwa ushindi wa jumla wa 3-2 baada ya awali kufungwa 1-0 nchini Afrika Kusini.
    TP Mazembe ilipata mabao yake kupitia kwa Rainford Kalaba dakika ya 36, Samatta dakika ya 45 na Rogger Assale dakika ya 57, wakati bao la kufutia machozi la Mamelodi Sundowns lilifungwa na Percey Tau dakika ya 84.
    TP Mazembe; Kidiaba, Frimpong, Kimwaki, Coulibaly, Kasusula/Singuluma dk59, Diarra, Adjei, Asante, Assale/Bolingi dk67, Samatta na Kalaba.
    Mamelodi Sundowns: Onyango, S. Zwane, Mphahlele, Schut, Mashaba, Kekana/Niang dk74, Zungu, Modise, T. Zwane/Laffor dk53, Malajila/Tau dk66 na Billiat.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SAMATTA AING’ARISHA MAZEMBE, YAENDA 16 BORA LIGI YA MABINGWA AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top