![]() |
| Rais wa TFF, Jamal Malinzi (kushoto) na Leodegar Tenga kulia |
Aidha Rais Malinzi ametuma salamu za pongezi kwa wajumbe waliochaguliwa kuwa wajumbe wapya wa Shirikisho la Mpira wa Miguu baranai Afrika (CAF) na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).
Katika salamu hizo na nakala zake kutumwa kwa Rais wa CAF, Issa Haytou na Rais wa FIF, Blatter, Malinzi amewatakia kila la kheri katika majukumu hayo mapya,na kwa ajili ya maendeleo ya mpira wa miguu duniani.
Tenga amechaguliwa nafasi hiyo baada ya kuwa mgombea pekee kutoka kanda ya Afrika Mashariki aliyejitokeza kuwania nafasi hiyo na kuungwa mkono na nchi zote wanachama wa CECAFA.



.png)
0 comments:
Post a Comment