YANGA SC itakutana na Etoile du Sahel ya Tunisia katika hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho Afrika katikati ya mwezi ujao.
Hiyo inafuatia Etoile kutoa sare ya 1-1 na Benfica de Luanda nchini Angola katika mchezo wa marudiano hatua ya 32 Bora leo.
Etoile imefuzu kwa ushindi wa jumla wa 2-1, baada ya awali kushinda 1-0 Tunis na sasa itasafiri hadi Dar es Salaam katikati ya Aprili kuja kucheza na Yanga, kabla ya timu hizo kurudiana mwanzoni mwa Mei.
Yanga SC imeitoa Platinum FC ya Zimbabwe kwa jumla ya mabao 5-2, ikishinda 5-1 nyumbani kabla ya kwenda kufungwa 1-0 ugenini.

.png)
0 comments:
Post a Comment