BONDIA mstaafu, Serafim Todorov, mtu wa mwisho kumshinda ulingoni Floyd Mayweather, sasa anaishi kwa mshahara wa dola za Kimarekani 370 kwa mwezi kutoka Serikali ya Bulgaria.
Mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 45, alimpiga Mayweather katika pambano la uzito wa Feather Nusu Fainali ya michuano ya Olimpiki mwaka 1996 mjini Atlanta, lakini leo maisha yake ni ‘mabovu’.
Nusu fainali hiyo iliisha kwa utata kutokana na refa kumuinua mkono juu kimakosa Mayweather, lakini Todorov ndiye aliyeshinda kwa pointi.
Serafim Todorov ndiye bondia wa mwisho kumpiga Floyd Mayweather katika michezo ya Olimpiki mwaka 1996 mjini Atlanta
Todorov (kushoto) anaishi katika 'kichovu' Bulgaria wakati Mayweather ni mmoja wa wanamichezo tajiri duniani
Todorov alipigwa na bondia wa Thailand, Somluck Kamsing katika Fainali ya Olimpiki mjini Atlanta 1996 na baada ya hapo akapigana mapambano sita tu ya ngumi za kulipwa, akishinda matano kati ya mwaka 1998 na 2003, kabla ya kupoteza moja mbele ya Toni Naskovski mjini Macedonia mwaka 1999.
Mmarekani Mayweather anajiandaa kwa moja ya mapambano ya kihistoria katika ulimwengu wa ndondi dhidi ya Mfilipino Manny Pacquiao litakalofanyika mjini Las Vegas, Mei 2 na amekwishapigana mapambano 47 katika ngumi za kulipwa bila kupoteza hata moja.
Kwa sasa Mayweather ni mwanamichezo tajiri zaidi duniani, wakati huo huo Todorov, anaishi katika nyumba moja ndogo mjini Pazardzhik, kusini mwa Bulgaria akichangia gari aina ya Volkswagen Polo na mkewe.
Mayweather kwa sasa ni mwanamichezo tajiri duniani na amekuwa akiposti picha za utajiri wake kwenye mitandao ya kijamii
“Naishi kwa msaada kidogo kutoka serikalini, lakini fedha ninazopata kutoka serikalini hazitoshi, familia yangu haina kazi. Ni vigumu hapa kwa sababu ni mji mdogo na kuna nafasi chache za kazi,”.
“Napata kama Euros 500 kwa mwezi, lakini nalazimika kulipa madeni benki au mikopo, namiliki nyumba ndogo (apartment) nayoishi, lakini hapa bado kuna bili za kulipa,” amesema.
“Nilikuwa nina nyumba kubwa nyumbani kwetu Peshtera, kilomita 20 kutoka hapa ninapoishi kwa sasa, lakini ilibidi niiuze kwa sababu sikuwa na fedha za kujikimu,” amesema.
Todorov (kulia) alipigwa na Somluck Kamsing katika fainali uzito wa Feather michezo ya Olimpiki mwaka 1996 mjini Atlanta


.png)
0 comments:
Post a Comment