Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
MSHAMBULIAJI wa Yanga SC, Mrisho Khalfan Ngassa amekanusha habari kwamba amesaini klabu ya Free State Stars ya Afrika Kusini, ingawa amekiri kufanya mazungumzo na klabu hiyo.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY jana mjini Dar es Salaam, Ngassa amesema kwamba tangu mwaka jana Free State wanamtaka, lakini hajafikia kutiliana saini na klabu hiyo.
“Nashangaa sana hizi habari, kwanza hata Free State kocha wao siyo Saintfiet (Tom), ni Phiri (Kinah). Yule Saintfiet alikwishaondoka na sasa yupo yule Phiri wa Malawi,”amesema Ngassa.
“Ni jambo zuri watu kama wanataka kuandika habari za mtu basi wakawasiliana naye. Na mimi nimekuwa nikitoa sana ushirikiano na vyombo vya habari.
“Huyu mtu anaandika hivi maana yake anataka kunichonganisha na klabu yangu au vipi? Ni kweli ninaweza kuondoka Yanga mwishoni mwa msimu nikimaliza Mkataba wangu. Lakini bado sijasaini popote,”.
“Basi wangewatafuta hata hao Free State wawaulize kama nimesaini kwao. Mtu anaandika kwa uhakika Ngassa kasaini hadi mshahara anapanga, hivi vitu siyo vizuri,”amesema Ngassa.
Nyota huyo wa Wana Jangwani amesema kwamba amefanya mazungumzo na klabu tatu hadi sasa, moja ya Qatar, nyingine ya Afrika Kusini na nyingine ya hapa nyumbani, lakini hajasaini popote.
“Hapa nyumbani nimefanya mazungumzo na klabu yangu, (Yanga). Wao wanataka nibaki na tunaendelea na mazungumzo. Lolote linaweza kutokea, mimi kama mchezaji naangalia maslahi. Kama Yanga watatoa ofa nzuri kwa nini niondoke?”amehoji Ngassa.
Ngassa anatarajiwa kumaliza Mkataba wake mwishoni mwa msimu na vyombo vya habari nchini vimekuwa vikiripoti tofauti kuhusu motto huyo wa kiungo wa zamani wa Simba SC, Khalfan Ngassa- zaidi vikimuhusisha na kuondoka Jangwani.

![]() |
| Mrisho Ngassa amekanusha kusaini Free State Stars ya Afrika Kusini |

.png)
0 comments:
Post a Comment