• HABARI MPYA

    Monday, April 06, 2015

    JONAS MKUDE AFIWA NA BABA MZAZI

    KIUNGO mkabaji wa Simba SC, Jonas Gerald Mkude ameondoka kwenye kambi ya Simba SC mjini Shinyanga Jumapili kurejea Dar es Salaam, kufuatia taarifa za kifo cha baba yake mzazi.
    Mzee Jonas Mkude amefariki dunia Jumapili jioni katika hospitali ya Mwananyamala, Dar es Salaam ambako alikuwa amelazwa tangu Alhamisi kwa matibabu ya figo.
    Simba SC sasa itakosa huduma ya Mkude katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Jumatatu jioni dhidi ya Kagera Sugar Uwanja wa Kaitaba, Shinyanga.
    Pole mchezaji; Kiungo Jonas Mkude amefiwa na baba yake mzazi, hivyo kulazimika kuiacha kambi ya Simba SC Shinyanga na kurejea Dar es Salaam 

    Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya SImba SC, Hajji Sunday Manara amesema kwamba uongozi umezipokea kwa masikitiko makubwa taarifa hizo.
    “Tunampa pole mchezaji wetu, kipenzi cha wapenzi wa Simba, Jonas Mkude na tunaahidi kuwa naye bega kwa bega katika kipini hiki kigumu kwake,”amesema.
    Aidha, Manara amesema kwamba tayari viongozi wa klabu waliopo Dar es Salaam wamekwishaanza kushughulikia suala hilo na mazishi yanatarajiwa kufanyika Jumatano.        
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: JONAS MKUDE AFIWA NA BABA MZAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top