PSG imetoka nyuma mara mbili kusawazisha mabao hadi kupata ushindi wa 3-2 dhidi ya mahasimu wao, Marseile katika mchezo wa Ligi Kuu ya Ufaransa, maarufu Ligue 1 usiku huu.
Andre-Pierre Gignac alianza kuifungia Marseille dakika ya 30 kwa kichwa cha nguvu akimalizia krosi ya Dimitri Payet, lakini Blaise Matuidi akaisawazishia PSG dakika tano baadaye.
Gignac akaifungia tena Marseille dakika ya 43- na Marquinhos akaisawazishia tena PSG dakika ya 49, kabla ya Jeremy Morel kujifunga kwa presha aliyopewa na Zalatan Ibrahimovic kuipatia bao la ushindi PSG dakika ya 51.
Kikosi cha Marseille kilikuwa; Mandanda, Romao, Fanni, Morel, Lemina, Dja Djedje, Mendy, Payet, Thauvin/Ocampos dk63, Gignac/Batshuayi dk71 na Ayew/Alessandrini dk72.
PSG: Sirigu, Marquinhos, Thiago Silva, David Luiz/Van der Wiel dk34, Maxwell, Verratti, Motta, Matuidi, Pastore/Rabiot dk82, Ibrahimovic na Cavani/Lavezzi dk59.
Zlatan Ibrahimovic (kushoto) akiwania mpira dhidi ya Jeremy Morel katika mchezo wa Ligue 1 Jumapili ya Pasaka
PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-3026741/Marseille-2-3-PSG-French-champions-twice-come-return-Ligue-1-brilliant-battle-Stade-Veledrome-David-Luis-injury-mars-victory.html#ixzz3WTWfvbwr


.png)
0 comments:
Post a Comment