• HABARI MPYA

    Monday, April 06, 2015

    BARCA YAZIDI KUWAACHA REAL MADRID MBIO ZA UBINGWA LA LIGA, YASHINDA 1-0 UGENINI

    BARCELONA imezidi kuikimbia Real Madrid kileleni mwa La Liga kufuatia ushindi wa 1-0 usuku huu dhidi ya Celta Vigo Uwanja wa Balaidos.
    Shukrani kwake, mfungaji wa bao hilo pekee, Jeremy Mathieu dakika ya 73 katika mchezo ambao Orellana alionyeshwa kadi nyekundu baada ya kumrushia nyasi Sergio Busquets. 
    Mshambuliaji wa Barcelona, Luis Suarez alionyeshwa kadi ya njano kwa kujirusha kumdaganya Vicandi Garrido.
    Kikosi cha Celta Vigo kilikuwa; Alvarez Conde, Mallo Novegil, Cabral, Fontas, Castro Otto, Hernandez, Fernandez, Krohn-Dehli/Radoja dk67, Orellana, Larrivey/Dias de Oliveira dk71 na Agudo Duran.
    Barcelona: Bravo, Dani Alves, Pique, Mathieu, Adriano, Rafinha/Xavi dk58, Busquets, Iniesta/Pedro dk75, Messi, Suarez/Rakitic dk85 na Neymar.
    The Frenchman wheels away in celebration of his second half header at the Balaidos Stadium
    Jeremy Mathieu akishangilia baada ya kufunga Uwanja wa Balaidos

    PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-3026762/Celta-Vigo-0-1-Barcelona-Jeremy-Mathieu-s-header-Luis-Enrique-s-Fabian-Orellana-sees-red-throwing-grass-Sergio-Busquets.html#ixzz3WTTasa72 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BARCA YAZIDI KUWAACHA REAL MADRID MBIO ZA UBINGWA LA LIGA, YASHINDA 1-0 UGENINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top