• HABARI MPYA

    Sunday, April 05, 2015

    EL MERREIKH 'WAIUMIZA ROHO' AZAM FC, WAENDA 16 BORA LIGI YA MABINGWA

    TIMU ya El Merreikh ya Sudan imeitoa Kabuscorp ya Angola katika hatua ya 32 Bora Ligi ya Mabingwa Afrika licha ya kufungwa 2-1 mjini Luanda jana.
    Matokeo hayo, yanaifanya Merreikh itinge hatua ya 16 Bora kwa ushindi wa jumla wa mabao 3-2, baada ya awali kushinda 2-0 nyumbani.
    Ikumbukwe, Merreikh ndiyo waliowatoa wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano hiyo, Azam FC kwa jumla ya mabao 3-2 pia.
    Mechi ya kwanza Dar es Salaam Azam FC walishinda 2-0 na marudiano Sudan, Merreikh wakashinda 3-0. 
    Kikosi cha El Merreikh kilichoitoa Azam FC Raundi ya Kwanza Ligi ya Mabingwa Afrika, kimeendelea kuchanja mbuga baada ya kutinga hatua ya 16 Bora michuano hiyo

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: EL MERREIKH 'WAIUMIZA ROHO' AZAM FC, WAENDA 16 BORA LIGI YA MABINGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top