BASI lililokuwa limebeba wachezaji wa timu ya Fenerbahce ya Uturuki na makocha wao, limeshambuliwa kwa risasi jana usiku.
Gavana wa Jiji la Trabzon, Abdulcelil Oz amesema kwamba dereva wa baso hilo alipigwa risasi, baada ya awali kufikiri alipigwa jiwe.
Televisheni ya Fenerbahce imesema baso hilo lilishambuliwa kwa mtutu wa bunduki. Walinzi wa usalama walikwenda haraka kuliokoa gari hilo baada ya dereva kupigwa risasi na wakafanikiwa kulisimamisha salama. Hakuna mchezaji aliyeumia.
Alama ya eneo ambalo ilipenya risasi katika kioo cha basi la Fenerbahce baada ya shambulio hilo 
Kioo cha karibu na dereva kilivunjika kabisa kwa shambulio hilo
"Hali halisi ya sasa ni kwamba basi lilishambulia kwa mtutu," amesema Oz. "Ni mapema mno kusema chochote cha kufafanua, lakini kilichotokea ni risasi iliyorushwa kutoka kwa bunduki,".
Kiungo wa zamani wa Liverpool, Dirk Kuyt alikuwa miongoni mwa wachezaji 40 na Maofisa waliokuwapo kwenye basi hilo lililoshambuliwa karibu na mji wa Trabzon.
Dereva wa basi alipata maumivu kichwani na akakimbizwa hospitali. Hakuna mchwzaji aliyejeruhiwa, klabu hiyo imethibitisha.
Shambulio hilo lilikuja saa kadhaa baada ya Fenerbahce kushinda mabao 5-1 dhidi ya timu ya Black Sea, Caykur Rizespor katika Super Lig ya Uturuki.
PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-3025939/Fenerbahce-team-coach-shot-armed-gang-way-away-game.html#ixzz3WPYy969V


.png)
0 comments:
Post a Comment