Mshambuliaji wa Chelsea, Diego Costa akitoka nje baada ya kuumia nyama za paja dakika ya 10 tangu aingie uwanjani akitokea benchi jana Chelsea ikishinda 2-1 dhidi ya Stoke City Uwanja wa Stamford Bridge, London.
Haijulikani The Blues itamkoa kwa muda gani haswa Costa, ingawa taarifa za awali zinasema si chini ya wiki mbili
Kuumia kwa Costa ni pigo kwa Chelsea katika hatua hizi za mwishoni za msimu, The Blues wakikabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa Manchester City, Manchester United na Arsenal katika mbio za ubingwa.


.png)
0 comments:
Post a Comment