• HABARI MPYA

  Saturday, May 01, 2021

  SIMBA SC YATOKA NYUMA NA KUICHAPA KAGERA SUGAR 2-1 NA KUTINGA ROBO FAINALI AZAM SPORTS FEDERATION CUP

  MABINGWA watetezi, Simba SC wametoka nyuma na kuichapa Kagera Sugar 2-1 katika mchezo wa Hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) usiku huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Kagera Sugar ilitangulia kwa bao la Erick Mwijage dakika ya 45, kabla ya Simba kutoka nyuma kwa mabao ya winga Mghana, Bernard Morrison dakika ya 56 na mshambuliaji Mnyarwanda, Meddie Kagere dakika ya 68.
  Simba inakuwa timu ya saba kwenda Robo Fainali baada ya Azam FC na Yanga SC, za Dar es Salaam pia, Biashara United ya Mara, Mwadui FC ya Shinyanga, Dodoma Jiji FC ya Dodoma na Rhino Rangers ya Tabora, timu pekee isiyo ya Ligi Kuu kufika hatua hiyo.
  Hatua ya 16 Bora ya ASFC itakamilishwa kesho kwa mchezo kati ya JKT Tanzania na Namungo FC Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YATOKA NYUMA NA KUICHAPA KAGERA SUGAR 2-1 NA KUTINGA ROBO FAINALI AZAM SPORTS FEDERATION CUP Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top