• HABARI MPYA

  Saturday, May 01, 2021

  DODOMA JIJI FC YATINGA ROBO FAINALI KOMBE LA TFF BAADA YA KUICHAPA KMC LEO UWANJA WA JAMHURI

  TIMU ya Dodoma Jiji FC imefanikiwa kutinga Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya KMC jioni ya leo Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
  Mabao ya Dodoma Jiji FC yamefungwa Seif Abdallah Karihe dakika ya 19 na Dickson Ambundo dakika ya 41 na sasa inaungana na Rhino Rangers ya Tabora, Biashara United ya Mara, Mwadui FC ya Shinyanga, Azam FC na Yanga za Dar es Salaam kutinga Nane Bora.
  Mchezo mwingine wa ASFC unaendelea hivi sasa Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam baina ya wenyeji na mabingwa watetezi, Simba SC na Kagera Sugar ya Bukoba.
  Hatua ya 16 Bora itakamilishwa kesho kwa mchezo kati ya wenyeji, JKT Tanzania na Namungo FC Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.

   
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: DODOMA JIJI FC YATINGA ROBO FAINALI KOMBE LA TFF BAADA YA KUICHAPA KMC LEO UWANJA WA JAMHURI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top