• HABARI MPYA

  Jumapili, Oktoba 28, 2018

  MMILIKI WA LEICESTER CITY AFARIKI DUNIA NDANI YA HELIKOPTA YAKE ILIYOTEKETEA KWA MOTO

  IMETHIBITISHWA mmiliki wa klabu ya Leicester City ya England, Vichai Srivaddhanaprabha amefariki dunia baada ya helikopta aliyokuwa amepanda kuteketea kwa moto.
  Mashabiki wa Leicester City wapo katika majonzi makubwa kufuatia taarifa kwamba mmiliki wa klabu yao, Srivaddhanaprabha alikuwepo kwenye helikopta iliyoteketea kwa moto baada ya kulipuka na kuungua nje ya Uwanja wa King Power mjini Leicester, Leicestershire jana. 
  Tukio hilo lilitokea dakika chache tu baada ya mchezo wa Ligi Kuu ya England jana, Leicester City wakilazimishwa sare ya kufungana bao na 1-1 West Ham, wageni wakitangulia kwa bao la Fabian  Balbuena dakika ya 30 kabla ya Wilfred Ndidi kuwasawazishia wenyeji, dakika ya 89.
  Polisi na klabu hiyo bado hawajatoa taarifa yoyote rasmi juu ya janga hilo, lakini Shirika la Utangazaji Uingereza (BBC) limeripoti kwamba mtu wa karibu wa bilionea huyo wa Thailand amesema Srivaddhanaprabha na watu wengine wanne wamefariki katika ajali hiyo.
  Walioshuhudia tukio hilo wanasema kwamba waliona helikopta hiyo inaungua muda mfupi tu baada ya kuruka kutoka uwanjani hapo. 

  Mashabiki wa Leicester City wakiwa nje ya Uwanja wa King Power kufuatia taarifa za kifo cha mmiliki wa klabu yao, Vichai Srivaddhanaprabha
    
  Taarifa za awali zilisema kwamba binti ya Srivaddhanaprabha alikuwepo kwenye helikopta hiyo wakati inateketea moto, ingawa Leicester FC wamekanusha madai hayo. 
  Mashabiki walishitushwa mno na tukio hilo na wengine waliangulia vya machozi baada ya ndege hiyo kuingizwa ndani ya Uwanja kwenye eneo la kuegeshea magari.
  Srivaddhanaprabha alikuwa mchora ramani wa taji la ubingwa wa Ligi Kuu ya England walilochukua Leicester katika msimu ambao walipanda kutoka Daraja la Kwanza, mwaka 2016.
  Aliibadilisha kabisa klabu hiyo baada ya kuinunua mwaka 2016 kwa dau la Pauni Milioni 39 mwaka 2010.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MMILIKI WA LEICESTER CITY AFARIKI DUNIA NDANI YA HELIKOPTA YAKE ILIYOTEKETEA KWA MOTO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top