• HABARI MPYA

  Jumatano, Oktoba 31, 2018

  MOHAMMED ISSA ‘BANKA’ KUANZA KUICHEZEA YANGA FEBRUARI 8 MWAKANI ADHABU YAKE YA BANGI IKIISHA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KIUNGO Mohammed Issa Juma 'Banka' ataruhusiwa kuendelea kucheza soka ifikapo Februari 8 mwakani atakapomaliza adhabu yake ya kufungiwa kucheza soka kwa miezi 14 kufuatia kukutwa na hatia ya kutumia dawa za kulevya.
  Kamati ya Kuzuia na Kupambana na Dawa Zisizoruhusiwa Michezoni ya Kanda ya Tano Afrika (RADO) ilimfungia kwa miezi 14 kiungo huyo wa kimataifa wa Tanzania baada ya kumkutana hatia ya kutumia mihadarati.
  Banka aliyesajiliwa Yanga SC Julai mwaka huu kutoka Mtibwa Sugar ya Morogoro, alikutwa na hatia ya kutumia dawa zilizopigwa marufuku michezoni, aina ya Bangi Desemba 9 mwaka jana baada ya kufanyiwa vipimo wakati wa michuano ya CECAFA Challenge nchini Kenya.

  Mohammed Issa 'Banka' (kulia) atarejea uwanjani Februari 8 mwakani akimaliza adhabu ya kufungiwa miezi 14

  Katika michuano hiyo, Banka aliisaidia Zanzibar kufika fainali baada ya kufunga bao la ushindi kwa penalti dakika ya 58 Heroes wakiilaza Uganda 2-1 Desemba 15 Uwanja wa Moi mjini Kisumu katika mchezo wa Nusu Fanali.
  Siku hiyo Zanzibar walitangulia kwa bao la Makame dakkka ya 23 kabla ya Derick Nsibambi kuisawazishia The Cranes dakika ya 29 na ndipo ‘Mo Banka’ akawazima Waganda kipindi cha pili. 
  Na kwenye fainali, pamoja na kucheza vizuri, Zanzibar wafungwa na wenyeji, Kenya kwa penalti 3-2 kufuatia sare ya 2-2 ndani ya dakika 120 Uwanja wa Kenyatta huko Machakos.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MOHAMMED ISSA ‘BANKA’ KUANZA KUICHEZEA YANGA FEBRUARI 8 MWAKANI ADHABU YAKE YA BANGI IKIISHA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top