• HABARI MPYA

  Friday, October 26, 2018

  SAMATTA AFUNGA MABAO MAWILI EUROPA LEAGUE GENK IKIICHAPA BESIKTAS 4-2 PALE PALE ISTANBUL

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta jana amefunga mabao mawili katika ushindi wa 4-2 dhidi ya wenyeji Besiktas kwenye mchezo wa Kundi I Europa League Uwanja wa Vodafone mjini Istanbul.
  Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Samatta alifunga mabao yake dakika za 23 na 69 na yote akitengenezewa nafasi na beki kinda Mdenmark mwenye umri wa miaka 21, Joakim Maehle.
  Mabao mengine ya Genk yalifungwa na viungo Dieumerci N'Dongala kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) dakika ya 81 na Mpoland Jakub Piotrowski dakika ya 83.
  Vágner Love ndiye aliyefunga mabao yote ya Besiktas la kwanza dakika ya 74 akimalizia pasi ya Gokhan Gonul na la pili dakika ya 86 akimalizia pasi ya Mustafa Pektemek.
  Mbwana Samatta jana amefunga mabao mawili katika ushindi wa 4-2 wa Genk dhidi ya Besiktas 

  Genk sasa inaongoza kundi I baada ya kufikisha pointi sita kufuatia kucheza mechi tatu, ikishinda mbili na kufungwa moja, inafuatiwa na Malmo FF yenye pointi nne sawa na Sarpsborg 08, wakati Besiktas yenye pointi tatu inashika mkia.  
  Samatta jana amefikisha mechi 124 katika mashindano yote tangu amejiunga na Genk Januari mwaka 2016 akitokea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na amefunga jumla ya mabao 47.
  Katika Ligi ya Ubelgiji amecheza mechi 96 na kufunga mabao 33, Kombe la Ubelgiji mechi nane mabao mawili na Europa League mechi 20 mabao 14.
  Kikosi cha Besiktas kilikuwa: Karius, Medel, Quaresma, Ozyakup, Lens, Tolgay/Roco dk26, Uysal, Vida, Gönül, Erkin/Ektemek dk84 na Larin/Vagner Love dk45.
  KRC Genk : Vukovic, Maehle, Dewaest, Lucumi, Uronen, Heynen, Malinovskyi, Pozuelo/Seck dk80, Ndongala, Paintsil/Piotrowski dk76 na Samatta/Gano dk87.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SAMATTA AFUNGA MABAO MAWILI EUROPA LEAGUE GENK IKIICHAPA BESIKTAS 4-2 PALE PALE ISTANBUL Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top