• HABARI MPYA

  Jumapili, Oktoba 28, 2018

  NGOMA AFUNGA BAO PEKEE NAMFUA AZAM YAICHAPA 1-0 SINGIDA UNITED, MTIBWA SUGAR NAO WAWAPIGA KAGERA

  Na Mwandishi Wetu, SINGIDA
  BAO pekee la mshambuliaji Mzimbabwe, Donald Dombo Ngoma limeipa ushinidi wa 1-0 Azam FC dhidi ya wenyeji, Singida United katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Namfua mjini Singida.
  Ngoma alifunga bao hilo dakika ya 29 kwa ufundi akimalizia pasi nzuri ya mshambuliaji, Yahya Zayed na Azam FC inafikisha pointi 27 katika mechi ya 11, ikiendelea kuongoza Ligi Kuu, ikifuatiwa na Simba SCyenye pointi 20 za mechi tisa na Yanga SC yenye pointi 19 za mechi saba. 
  Mechi nyingine za Ligi Kuu leo, bao pekee la Juma Luizio dakika ya 87 limeipa ushindi wa 1-0 Mtibwa Sugar dhidi ya Kagera Sugar ya Bukoba Uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro leo.
  Nayo Alliance FC imelazimishwa sare ya kufungana 1-1 na Coastal Union ya Tanga Uwanja wa Nyamagana mjini Mwanza. Deogratias Anthony alianza kuifungia Coastal Union dakika ya 45 na ushei, kabla ya Hance Masoud kuisawazishia Alliance dakika ya 54.

  Donald Ngoma akipongezwa na wenzake baada ya kufunga bao pekee katika ushinidi wa 1-0 dhidi ya Singida United leo

  Na Uwanja wa Meja Isamhuyo, Mbweni bao pekee la Anuary Kilemile dakika ya 78 limeipa ushindi wa 1-0 JKT Tanzania dhidi ya Tanzania Prisons.
  Mechi ya mwisho ya Ligi Kuu leo inafuatia hivi sasa Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam kati ya Ruvu Shooting na mabingwa watetezi, Smba SC.
  Baada ya hapo, Ligi Kuu itaendelea kesho kwa mechi mbili, Stand United na mahasimu wao wa Jiji la Shinyanga, Mwadui FC na African Lyon na Biashara United Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam kuanzia Saa 10:00 jioni.
  Jumanne, Mbao FC wataikaribisha Mbeya City Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza kuanzia Saa 10:00 jioni na Yanga SC itaikaribisha Lipuli FC kuanzia Saa 1:00 usiku Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na Jumatano KMC FC watakuwa weyeji wa Ndanda FC.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: NGOMA AFUNGA BAO PEKEE NAMFUA AZAM YAICHAPA 1-0 SINGIDA UNITED, MTIBWA SUGAR NAO WAWAPIGA KAGERA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top