• HABARI MPYA

  Monday, October 22, 2018

  TFF YAZIBA NAFASI YA KUULI KAMATI YA UCHAGUZI, YAWATEUA PIA MUSSA AZZAN ‘ZUNGU’ NA ASP NYAGABONA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limeziba nafasi ya Mwenyekiti wa Kamati yake ya Uchaguzi iliyoachwa wazi na Revocatus Kuuli aliyejiuzulu mwezi uliopita kwa kumteua Malangwe Ally. 
  Msemaji wa TFF, Clifford Ndimbo amesema leo katika mkutano na Waandishi wa Habari mjini Dar es Salaam kwamba Kama ya Utendaji imefanya mabadiliko ya baadhi ya kamati zake kufuatia baadhi ya wajumbe na viongozi kujiuzulu.

  Mussa Azzan ‘Zungu’ ameteuliwa kuwa Mjumbe wa Kamati ya Rufaa Maadili ya TFF chini ya Mwenyekiti Richard Mbaruku  

  Na Malangwe Ally anachukua nafasi ya Kuuli aliyeng’atuka baada ya kutofautiana na Katibu Mkuu wa TFF, Wilfred Kidau.
  Malangwe atafanya kazi na Makamu Mwenyekiti Mohamed Mchengerwa na Wajumbe Benjamin Karume, Mohamed Gombati na Hamisi Zayumba.
  Mabadiliko hayo yamegusa na Kamati ya Nidhamu pia, ambayo sasa Mwenyekiti wake anakuwa Kiomoni Kibamba, Makamu Peter Hella na Wajumbe Kassim Dau, Handley Matwenga na Twaha Mtengera.
  Katika Kamati ya Rufaa Maadili, Richard Mbaruku anakuwa Mwenyekiti, Thadeus Karua Makamu Mwenyekiti na Wajumbe Mussa Azzan ‘Zungu’, ASP Benedict Nyagabona na Lugano Hosea.
  Wakati huo huo: Mkutano Mkuu wa Mwaka wa TFF umepangwa kufanyika Desemba 29, mwaka huu mjini Arusha.
  Uamuzi huo umepitishwa na kikao cha Kamati ya Utandaji ya TFF kilichofanyika Oktoba 20 mwaka huu na kutangazwa leo ikiwa ni zaidi ya siku 60 kabla ya tarehe ya mkutano kwa mujibu wa Katika ya TFF
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TFF YAZIBA NAFASI YA KUULI KAMATI YA UCHAGUZI, YAWATEUA PIA MUSSA AZZAN ‘ZUNGU’ NA ASP NYAGABONA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top