• HABARI MPYA

  Sunday, October 21, 2018

  MSUVA AIFUNGIA BAO LA KUFUTIA MACHOZI DIFAA HASSAN EL - JADIDI IKICHAPWA 2-1 UGENINI MOROCCO

  Na Mwandishi Wetu, MARRAKECH
  WINGA wa kimataifa wa Tanzania, Simon Msuva jana alitokea benchi na kuifungia bao la kufutia machozi dakika ya 62 klabu yake, Difaa Hassan El Jadidi ikichapwa 2-1 na wenyeji Kawkab Marrakech katika mchezo wa Ligi Kuu ya Morocco, maarufu kama Botola Pro Uwanja wa Marrakech.
  Hapana shaka ni kutokana na uchovu Msuva jana alianzia benchi, kwani ni Jumanne tu alikuwa Dar es Salaam kuichezea timu yake ya taifa, Tanzania katika mchezo wa Kundi L kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwakani nchini Cameroon dhidi ya Cape Verde.
  Simon Msuva akimtoka bekiwa Kawkab Marrakech jana katika mchezo wa Ligi Kuu ya Morocco Uwanja wa Marrakech

  Simon Msuva akiwa benchi kabla ya kuingia jana dhidi ya Kawkab Marrakech Uwanja wa Marrakech

  Na siku hiyo, Msuva alifunga bao la kwanza dakika ya 29 katika ushindi wa 2-0 Uwanja wa Taifa kabla ya Nahodha Mbwana Samatta kufunga la pili dakika ya 58.  
  Mechi nyingine za Ligi Kuu Morocco jana, Khouribga ililazimishwa sare ya 1-1 na Raja Casablanca sawa na Ittihad Tanger ambayo nayo ilitoka 1-1 na Chabab Rif Hoceima.
  Pamoja na matokeo hayo, Difaa Hassan El-Jadidi inaendelea kuongoza Ligi ya Morocco kwa pointi zake tisa baada ya kucheza mechi nne, ikishinda tatu na kupoteza moja, ikifuatiwa na Kawkab Marrakech na Olympic Safi ambazo zote kila moja ina pointi saba za mechi nne.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MSUVA AIFUNGIA BAO LA KUFUTIA MACHOZI DIFAA HASSAN EL - JADIDI IKICHAPWA 2-1 UGENINI MOROCCO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top