• HABARI MPYA

  Jumanne, Oktoba 30, 2018

  KOCHA WA TIMU B ARITHISHWA MIKOBA YA LOPETEGUI ALIYEFUKUZWA REAL MADRID

  KLABU ya Real Madrid imemfukuza kocha wake, Julen Lopetegui na kumpandisha kocha wa timu B, Santiago Solari kuiongoza timu kwa muda.
  Bodi ya Madrid imetofautiana juu ya mbadala wa Lopetegui. Rais, Florentino Perez anamtaka kocha wa zamani wa Chelsea, Antonio Conte lakini mahitaji yake ya mkataba wa miaka miwili na nusu ikiwemo wasaidizi hadi watano, vinaweza kumfanya kocha wa Ubelgiji, Roberto Martinez achukue nafasi kiulaini.
  Klabu pia inafikiria kumuacha Solari aendelee an kazi hadi mwezi ujao wakati wa mapumziko ya mechi za kimataifa itakapofanya uteuzi wa mwalimu wa kudumu.

  Real Madrid imemfukuza Julen Lopetegui baada ya kipigl cha 5-1 kwenye El Clasico Jumapili 

  Conte hakubaliki na wachezaji wa sasa na Nahodha, Sergio Ramos amesema: "Heshima inahitaji kuwepo, na si kuletwa," alisema aliopoulizwa juu ya uteuzi wa kocha asiyependa utovu wa nidhamu.
  Kocha wa zamani wa Everton na Wigan, Martinez ana nafasi ya kurejea kwenye klabu hiyo baada ya kufika Nusu Fainali kwenye Kombe la Dunia akiwa na Ubelgiji.
  Klabu pia inafikiria juu ya Conte kutofautiana na Eden Hazard, ambaye inataka kumchukua msimu ujao kama ataendelea kugoma kusaini mkataba mpya Chelsea.
  Conte ameshinda mataji ya Ligi Italia na England, lakini ukali wake ulisababisha atofautiane na wachezaji tegemeo wa Chelsea, Diego Costa na Hazard ambao walichoshwa na kuchezeshwa nje ya nafasi zao.
  Yeyote atayechukuliwa atakuwa kocha wa tano wa Gareth Bale katika miaka yake mitano ya kuwa na klabu hiyo ya Hispania.
  Lopetegui alitambulishwa kuwa kocha mpya wa Real Madrid Juni 14 baada ya kufukuzwa timu ya taifa ya Hispania kufuatia kuvuja kwa habari za yeye kujiunga na klabu hiyo huku akiwa na timu ya taifa nchni urusi.
  Lakini katika mechi 14 alizoiongoza timu, ameshinda sita tu. Mwalimu huyo mwenye umri wa miaka 52 anaiacha timu ikiwa nafasi ya tisa kwenye msimamo wa La Liga baada ya kipigo cha 5-1 Jumapili kutoka kwa Barcelona Uwanja wa Camp Nou.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KOCHA WA TIMU B ARITHISHWA MIKOBA YA LOPETEGUI ALIYEFUKUZWA REAL MADRID Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top