• HABARI MPYA

  Sunday, October 28, 2018

  HELIKOPTA YA MMILIKI WA LEICESTER CITY YATEKETEA MOTO NJE YA UWANJA

  HELIKOPTA ya mmiliki wa klabu ya Leicester City ya England, Vichai Srivaddhanaprabha jana iliteketea kwa moto baada ya kulipuka na kuungua nje ya Uwanja wa King Power mjini Leicester, Leicestershire.
  Tukio hilo lilitokea dakika chache tu baada ya mchezo wa Ligi Kuu ya England jana, Leicester City wakilazimishwa sare ya kufungana bao na 1-1 West Ham, wageni wakitangulia kwa bao la Fabian  Balbuena dakika ya 30 kabla ya Wilfred Ndidi kuwasawazishia wenyeji, dakika ya 89.
  Walioshuhudia tukio hilo wanasema kwamba waliona helikopta hiyo inaungua muda mfupi tu baada ya kuruka kutoka uwanjani hapo. 

  Helikopta ya mmiliki wa Leicester, Vichai Srivaddhanaprabha ikiteketekea kwa moto nje ya Uwanja wa King Power jana 

  Lakini chanzo cha kulipuka kwa helikopta hiyo inaelezwa na hitilafu za kwenye injini.
  Mashabiki walishitushwa mno na tukio hilo na wengine waliangulia vya machozi baada ya ndege hiyo kuingizwa ndani ya Uwanja kwenye eneo la kuegeshea magari.
  Haijulikani akina nani walikuwepo kwenye chombo hicho wakati kinateketea kwa moto, lakini mmiliki wa Leicester mwenyewe alikuwa anaangalia mechi.
  Srivaddhanaprabha alikuwa mchora ramani wa taji la ubingwa wa Ligi Kuu ya England walilochukua Leicester katika msimu ambao walipanda kutoka Daraja la Kwanza, mwaka 2016.
  Aliibadilisha kabisa klabu hiyo baada ya kuinunua mwaka 2016 kwa dau la Pauni Milioni 39 mwaka 2010.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: HELIKOPTA YA MMILIKI WA LEICESTER CITY YATEKETEA MOTO NJE YA UWANJA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top