• HABARI MPYA

  Thursday, October 25, 2018

  STAND UNITED WAMALIZIA HASIRA ZAKE KWA MTIBWA SUGAR, NDANDA FC NA MBEYA CITY NAZO ZANG’ARA NYUMBANI

  Na Mwandishi Wetu, SHINYANGA
  TIMU ya Stand United imemaliza hasira zake za kufungwa na Simba SC wiki iliyopita kwa kuichapa Mtibwa Sugar ya Morogoro mabao 2-1 jioni ya leo katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga.
  Mabao yote ya Stand United leo yamefungwa na Nahodha wake, Jacob Massawe dakika za 49 na 71, wakati la Mtibwa Sugar limefungwa na Ismail Mhesa dakika ya 64.
  Kwa ushindi huo, Stand United inafikisha pointi 14 baada ya kucheza mechi 11 na kupanda hadi nafasi ya 11 kutoka ya 13, wakati Mtibwa Sugar baada ya kupoteza mechi ya pili mfululizo Kanda ya Ziwa, kufuatia kufungwa pia na Mbao FC mjini Mwanza, wanabaki na pointi zao 17 baada ya kucheza mechi 11. 
  Stand United wamemaliza hasira zao za kufungwa na Simba SC kwa kuichapa Mtibwa Sugar leo

  Mechi nyingine za Ligi Kuu leo, bao la dakika ya pili la mshambuliaji Eliud Ambokile limeipa ushindi wa 1-0 Mbeya City dhidi ya Mwadui FC ya Shinyanga Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
  Nayo Ndanda FC imeibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Biashara United ya Mara Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara leo. Mabao ya Ndanda yamefungwa na Vitalis Mayanga dakika ya 19 na Ismail Mussa dakika ya 48, wakati la Biashara United limefungwa na Jerome Lambele dakika ya 71. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: STAND UNITED WAMALIZIA HASIRA ZAKE KWA MTIBWA SUGAR, NDANDA FC NA MBEYA CITY NAZO ZANG’ARA NYUMBANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top