• HABARI MPYA

  Jumatano, Oktoba 24, 2018

  SERENGETI BOYS YAINGIA KAMBINI KUJIANDAA NA MICHUANO YA COSAFA U17 ITAKAYOFANYIKA BOTSWANA DESEMBA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  TIMU ya taifa ya vijana ya Tanzania chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys imeingia kambini kujiandaa na mashindano ya Kombe la Mataifa ya Kusini mwa Afrika (COSAFA) U17 yanayotarajiwa kufanyika Desemba mwaka huu nchini Botswana.
  Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Clifford Mario Ndimbo amesema leo kwamba Serengeti Boys ipo kambini tangu Jumapili katika hosteli za shirikisho hilo, Uwanja wa Karume uliopo Ilala mjini Dar es Salaam.
  Ndimbo amesema kwamba kikosi kipo chini ya Kocha Mkuu, Oscar Milambo anayesaidiwa Maalim Saleh ‘Romario’ na kocha wa makipa, Manyika Peter.

  Ofisa Habari huyo amesema kwamba michuano hiyo ni sehemu ya maandalizi ya Fainali za Afrika za U17 mwakani, ambazo Tanzania ni mwenyeji.
  TFF imekuwa katika jitihada za kuitafutia Serengeti Boys mechi ngumu za kujipima nguvu kabla ya kuanza kwa fainali za AFCON U17 katikati ya mwakani.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SERENGETI BOYS YAINGIA KAMBINI KUJIANDAA NA MICHUANO YA COSAFA U17 ITAKAYOFANYIKA BOTSWANA DESEMBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top