• HABARI MPYA

  Wednesday, October 31, 2018

  KOCHA PAWASA ATAJA KIKOSI CHA FAINALI ZA AFRIKA SOKA LA UFUKWENI KASEJA NA MUSSA MGOSI NDANI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KOCHA Mkuu wa timu ya taifa ya soka la ufukweni, Boniface Pawasa ametaja kikosi chake kwa ajili ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zinazotarajiwa kuanza Desemba 8 hadi 14 mwaka huu nchini Misri.
  Katika kikosi hicho, Pawasa amewajumuisha wanasoka wenzake wa zamani wa kimataifa nchini, kipa Juma Kaseja na mshambuliaji Mussa Hassan Mgosi aliowika nao klabu ya Simba ya Dar es Salaam.
  Pamoja na Kaseja na Mgosi ambao bado wanacheza soka ya kawaida ya ushindani, wengine ni Ibrahim Abdallah, Ahmed Juma, Juma Ibrahim, Rolland Msonjo, Samuel Salonge, Yahya Tumbo na Jaruph Juma.  Kipa Juma Kaseja atakiongoza kikosi cha soka ya ufukweni Misri Desemba kwenye fainali za Afrika

  Wamo pia Ahmada Ahmada, Soud Ame Soud, Alfa Tindise, Kashiru Salum, Ali Humud Badru, Mohammed Makame, Shaffi Mussa, Justin Anthony na Seif Mwinyi.    
  Tanzania imepangwa kundi B pamoja na Senegal, Nigeria na Libya, wakati Kundi A likiwa na timu za Misri, Morocco, Ivory Coast na Madagascar.
  Hii ni mara ya kwanza kwa Tanzania kufuzu fainali hizo tangu ianzishe timu ya soka la ufukweni na imefuzu baada ya Afrika Kusini kujitoa kwenye safari ya kusaka tiketi hiyo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KOCHA PAWASA ATAJA KIKOSI CHA FAINALI ZA AFRIKA SOKA LA UFUKWENI KASEJA NA MUSSA MGOSI NDANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top