• HABARI MPYA

  Sunday, October 21, 2018

  SAMATTA AISAIDIA KRC GENK KUENDELEZA WIMBI LA USHINDI LIGI YA UBELGIJI, WASHINDA 2-1

  Na Mwandishi Wetu, GENK
  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta usiku wa jana aliisaidia timu yake, KRC Genk kuibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya AS Eupen katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza A Ubelgiji Uwanja wa Luminus Arena mjini Genk.
  Samatta alicheza vizuri jana akishirikiana na mshambuliaji kinda Mbelgiji Leandro Trossard mwenye umri wa miaka 23 kabla ya kupumzishwa dakika ya 81 kumpisha kumpisha kinda Mdenmark mwenye umri wa miaka 22, Marcus Ingvartsen.
  Na aliondoka uwanjani wakati amekwishamsaidia Trossard kufunga mabao yote mawili ya Genk dakika za 18 na 65, wakati la AS Eupen lilifungwa na beki Mfaransa mwenye umri wa miaka 22, Cheick Keita dakika ya 81.

  Mbwana Samatta akimpongeza mshambuliaji mwenzake, Mbelgiji Leandro Trossard baada ya kufunga mabao yote ya Genk

  Samatta jana amefikisha mechi 123 katika mashindano yote tangu amejiunga na Genk Januari mwaka 2016 akitokea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na amefunga jumla ya mabao 47.
  Katika Ligi ya Ubelgiji amecheza mechi 96 na kufunga mabao 33, Kombe la Ubelgiji mechi nane mabao mawili na Europa League mechi 19 mabao 12.
  Ikumbukwe, Jumanne wiki hii Samatta aliisaidia nchi yake, Tanzania kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Cape Verde kwenye mchezo wa Kundi L Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam. 
  Siku hiyo, Samatta alimsetia kiungo mshambuliaji wa Difaa Hassan El Jadidi ya Morocco Simon Msuva kufunga bao la kwanza kipindi cha kwanza kabla yay eye mwenyewe kufunga la pili kipindi cha pili.
  Kikois cha KRC Genk jana kilikuwa: Vukovic, Maehle, Aidoo, Dewaest, Urones, Heynen, Malinovskyi, Pozuelo, Ndongala/Paintsil dk65, Trossard/Seck dk86 na Samatta/Ingvartsen dk81.
  KAS Eupen : Van Crombrugge, Keita, Mulumba/Amani dk58, Garcia, Marreh, Toyokawa/Loties dk91, Blondelle, Gnaka/Essende dk82, Bushiri, Molina na Fall.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SAMATTA AISAIDIA KRC GENK KUENDELEZA WIMBI LA USHINDI LIGI YA UBELGIJI, WASHINDA 2-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top