• HABARI MPYA

  Jumapili, Oktoba 21, 2018

  HIMID MAO AINGIA DAKIKA YA 88 PETROJET YAPATA SARE 1-1 UGENINI, MAUMIVU YAMTESA BANDA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KIUNGO wa kimataifa wa Tanzania, Himid Mao Mkami jana alitokea benchi zikiwa zimesalia dakika mbili kuchukua nafasi ya Mhabeshi, Shimeles Bekele Godo timu yake, Petrojet ikilazimisha sare ya 1-1 ugenini na wenyeji, Al Ittihad katika mchezo wa Ligi Kuu ya Misri Uwanja wa Alexandria.
  Na Bekele aliondoka uwanjani akiwa ameifungia Petrojet bao la kusawazisha dakika ya 61, baada ya mshambuliaji Muivory Coast, Razack Cisse kutanguliwa kuwafungia wenyeji dakika ya 27.
  Himid hakuanzishwa jana kwa sababu wiki hii hakuwepo Misri kufuatia kuruhusiwa kwenda kuitumikia timu yake ya taifa, Taifa Stars katika mchezo wa Kundi L kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika mwakani nchini Cameroon Cameroon. 
  Himid Mao (kushoto) Jumanne aliisaidia Tanzania kushinda 2-0 dhidi ya Cape Verde
   

  Kwa upande mwingine, beki wa kimataifa wa Tanzania, Abdi Hassan Banda jana hakuwepo hata benchi wakati timu yake, Baroka FC inaibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Golden Arrows kwenye mchezo wa Kombe la Ligi Afrika Kusini Uwanja wa Pietersburg mjini Polokwane.
  Inawezekana ni maumivu yalimuweka benchi Banda, kwani Jumanne hakumaliza mechi akiichezea Tanzania dhidi ya Cape Verde katika mchezo wa Kundi L kufuzu AFCON ikishinda 2-0 Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
  Mabao ya Baroka FC yalifungwa na Collins Makgaka dakika ya kwanza akimalizia pasi ya Mtswana Onkabetse Makgantai na Tebogo Sodi dakika ya 79 akimalizia pasi ya Talent Chawapiwa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: HIMID MAO AINGIA DAKIKA YA 88 PETROJET YAPATA SARE 1-1 UGENINI, MAUMIVU YAMTESA BANDA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top