• HABARI MPYA

  Jumatano, Oktoba 31, 2018

  KMC YAISHINDILIA NDANDA FC 3-0 NA KUJIINUA KIDOGO KUTOKA CHINI KWENYE MSIMAMO WA LIGI KUU

  TIMU ya Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni (KMC) leo imebuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Ndanda FC ya Mtwara katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam. 
  Ushindi huo unaifanya KMC ifikishe pointi 13 baada ya kucheza mechi 12 na kupanda hadi nafasi ya 12 kwenye msimamo wa Ligi Kuu kutoka ya 15, wakati Ndanda inayobaki na pointi zake 12 baada ya kucheza mechi 12 inashuka kwa nafasi moja hadi ya 15.
  Katika mchezo wa leo, mabao ya KMC iliyopanda Ligi Kuu msimu huu, yamefungwa na Omar Ramadhani dakika ya 14 na James Msuva mawili, dakika za 60 na 76.

  KMC inayofundishwa na kocha Mrundi, Ettienne Ndayiragijje ambaye misimu miwili iliyopita alikuwa na Mbao FC ya Mwanza ilicheza vizuri na ilistahili ushindi huo mnono.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KMC YAISHINDILIA NDANDA FC 3-0 NA KUJIINUA KIDOGO KUTOKA CHINI KWENYE MSIMAMO WA LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top