• HABARI MPYA

  Jumatatu, Oktoba 29, 2018

  MSEMAJI WA SIMBA SC, HAJJI SUNDAY MANARA ATEULIWA KUWA BALOZI WA KAMPUNI YA ASAS YA IRINGA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MKUU wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba, Hajji Sunday Manara "De le Boss", amesema atahakikisha anaitendea haki heshima aliyopewa ya kuwa balozi wa Kampuni ya Asas ya mjini Iringa.
  Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Manara, alisema anaushukuru uongozi wa Asas kwa kumteua kuwa balozi wao na anaahidi kwa kutupia uwezo na vipaji alivyonavyo, atazinyanyua thamani za bidhaa zinazotengenezwa na kampuni hiyo.
  Manara alisema kuwa anawaomba mashabiki wa timu zote za soka hapa nchini kuhakikisha inatumia bidhaa hizo ili waweze kuimarisha afya zao na kufurahia mchezo huo wanaoupenda ambao unawakutanisha watu wa kada mbalimbali.
  Mwakilishi wa Asas, Jimmy Kiwelu (kulia), akimkabidhi Hajji Manara (kushoto) utambulisjo wa Ubalozi wa kampuni hiyo ya Iringa
  Mwakilishi wa Asas, Jimmy Kiwelu (kulia), akimkabidhi Hajji Manara (kushoto) utambulisjo wa Ubalozi wa kampuni hiyo ya Iringa 

  "Nitahakikisha kila kitu ambacho Asas watataka niwafanyie ninafanya, na itajulikana zaidi, nitajitahidi kuhakikisha bidhaa zao zinapatikana katika kila nyumba kwa sababu zinatumiwa na watu wote kuanzia watoto," alisema Manara.
  Naye Mwakilishi wa Asas, Jimmy Kiwelu, alisema kuwa kampuni yao ilifikia uamuzi wa kumteua Manara kutokana na kufahamu vyema uwezo na ushawishi alionao kwa jamii.
  "Tuliangalia mambo mbalimbali, ndio tukafikia uamuzi wa kusema Manara anatufaa, tutakuwa naye kwa muda wa miaka miwili," alisema Kiwelu.
  Meneja wa Manara, Beatrice, Ndowu, alisema kuwa anashukuru kufikia hatua hiyo na anaahidi kuendelea kumtafutia zaidi kazi huku kuahidi yoyote ambaye atafanya kazi na msemaji huyo wa Simba atakuwa amechagua sehemu sahihi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MSEMAJI WA SIMBA SC, HAJJI SUNDAY MANARA ATEULIWA KUWA BALOZI WA KAMPUNI YA ASAS YA IRINGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top