• HABARI MPYA

  Sunday, October 28, 2018

  PROMOTA MSANGI ADAI MFAUME MFAUME ALIONEWA NA REFA AKIPIGWA TKO RAUNDI YA PILI JANA URUSI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  PROMOTA Jay Msangi amesema bondia wake, Mfaume Mfaume alionewa na refa akipoteza pambano lake na Vaghinak Tamrazyan kwa Technical Knockout (TKO) raundi ya pili jana nchini Urusi.
  Katika taarifa yake aliyoituma kutoka nchini Urusi, Msangi amesema kwamba matokeo hayo hayakuwa halali kwa kuwa mwamuzi hakutenda haki kwani alimaliza pambano katika kipindi ambacho Mfaume alikuwa tayari kuendelea licha ya kuhesabiwa kuanzia moja hadi saba.
  “Wadau wa michezo tumepoteza pambano, bondia Mfaume Mfaume kapoteza pambano mapema baada ya kwenda chini raundi ya pili na refa kumhesabia na Mfaume kuinuka, ilipofika saba na Mfaume akiwa tayari kuendelea na pambano na akiwa katika hali nzuri bila madhara yeyote,". "Kwa mshituko mkubwa refa aliamua kumaliza pambano na kiwashangaza wadau wote ukumbini na hata kumuacha bondia Mtanzania akilia juu ya ulingo kwa machungu akiwa haelewi kwa nini refa amemaliza mapema”, amesema Msangi.

  Bondia Mfaume Mfaume akiwa safarini kurejea nyumbani baada ya kupoteza pambano kwa TKO raundi ya pili jana nchini Urusi

  Msangi amesema kwamba baada ya kupoteza pambano hilo la uzito Welter, Mfaume atakapowasili nchini alfajiri ya kesho Jumatatu atakuwa na mzungumzo na waandishi wa habari kuwafahamisha yaliyojiri katika pambano hilo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: PROMOTA MSANGI ADAI MFAUME MFAUME ALIONEWA NA REFA AKIPIGWA TKO RAUNDI YA PILI JANA URUSI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top