• HABARI MPYA

  Jumatano, Oktoba 24, 2018

  AZAM FC YAZIDI KUPAA LIGI KUU, LIPULI YAICHAPA MBAO 3-1 MWANZA…NA RUVU SHOOTING WAIPAPASA SINGIDA UNITED MLANDIZI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  BAO pekee la Yahya dakika ya 53 limetosha kuipa Azam FC ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, JKT Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Meja Isamuhyo huko Mbweni mjini Dar es Salaam.
  Ushindi huo unaifanya Azam FC ifikishe pointi 24 baada ya kucheza mechi 10, hivyo kuendelea kuongoza Ligi Kuu, ikifuatiwa na Yanga na Simba SC. 
  Katika mchezo mwingine wa Ligi Kuu, Lipuli FC imeifanyizia Mbao FC kwa kuichapa mabao 3-1 Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza.

  Mabao ya Lipuli yamefungwa na Issa Rashid dakika ya tisa, Zawadi Mauya dakika za 14 na 39, wakati la Mbao FC limefungwa na Said Khamis Jr. dakika ya 76 kwa penalti.
  Coastal Union ikalazimishwa sare ya 1-1 na Kagera Sugar Uwanja wa Mkwakwani, Tanga wenyeji wakitangulia kwa bao la Mohammed Mussa dakika ya pili kabla ya David Luhende kuwasawazishia wageni dakika ya 22.  
  Ruvu Shooting nayo imeichapa Singida United mabao 3-1  Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani.
  Tanzania Prisons imeendelea kusuasua baada ya kulazimishwa sare ya 0-0 na African Lyon Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: AZAM FC YAZIDI KUPAA LIGI KUU, LIPULI YAICHAPA MBAO 3-1 MWANZA…NA RUVU SHOOTING WAIPAPASA SINGIDA UNITED MLANDIZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top