• HABARI MPYA

  Jumanne, Oktoba 30, 2018

  TFF KUSAFIRISHA WAANDISHI WA HABARI 15 KWA BASI KWENDA KURIPOTI MECHI YA TAIFA STARS NA LESOTHO

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limetoa nafasi 15 za usafiri wa basi kwa Waandishi wa Habari kwenda Lesotho katikati ya mwezi ujao kwa ajili ya mchezo wa kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON).
  Tanzania watakuwa wageni wa Lesotho Novemba 18 katika mchezo wa Kundi L kufuzu AFCON ya mwakani nchini Cameroon, wakihitaji ushindi kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kufuzu.
  Ofisa Habari wa TFFm Clifford Ndimbo amesema leo mjini Dar es Salaam kwamba shirikisho litatoa usafiri wa basi kwa Waandishi wa Habari za Michezo kwenda na kurudi Lesotho, lakini watajigharamia kula na malazi.

  Vigogo wa TFF wakiwa katika picha ya pamoja na Waandishi wa Habari

  “Gharama nyingine zote za Visa, malazi, Chakula na nyingine zisizohusu usafiri itakuwa gharama ya msafiri mwenyewe (Mwandishi/Chombo). Nafasi zipo 15, safari itaanza Novemba 13,2018, kwa anayetaka kwenda afanye mawasiliano kupitia na Idara ya Habari ya TFF,” amesema Ndimbo.
  TFF pamoja na kutaka mashabiki wasafiri kwa wingi kwenda kuisapoti timu, lakini inawasaidia na Waandishi wa Habari waweze kwenda kuripoti mchezo huo muhimu unaoweza kuw awa kihistoria Taifa Stars ikishinda. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: TFF KUSAFIRISHA WAANDISHI WA HABARI 15 KWA BASI KWENDA KURIPOTI MECHI YA TAIFA STARS NA LESOTHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top