• HABARI MPYA

  Jumapili, Oktoba 28, 2018

  TANZANIA YAPANGWA KUNDI MOJA NA SENEGAL, NIGERIA NA LIBYA FAINALI ZA AFRIKA SOKA LA UFUKWENI

  Na Mwandishi Wetu, CAIRO
  TANZANIA imepangwa Kundi katika Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Soka la Ufukweni (Beach Soccer) zinazotarajiwa kuanza Desemba 8 hadi 14 mwaka huu nchini Misri.
  Katika droo iliyofanyika leo nchini Misri, Tanzania imepangwa kundi moja na Senegal, Nigeria na Libya, wakati Kundi A likiwa na timu za Misri, Morocco, Ivory Coast na Madagascar.
  Hii ni mara ya kwanza kwa Tanzania kufuzu fainali hizo tangu ianzishe timu ya soka la ufukweni na imefuzu baada ya Afrika Kusini kujitoa kwenye safari ya kusaka tiketi hiyo.

  Mechi zote za michuano hiyo inayoanza kujipatia umaarufu mkubwa barani Afrika zitafanyika mjini Sharm El Sheikh nchini Misri.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: TANZANIA YAPANGWA KUNDI MOJA NA SENEGAL, NIGERIA NA LIBYA FAINALI ZA AFRIKA SOKA LA UFUKWENI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top