• HABARI MPYA

  Monday, October 29, 2018

  WATANO WAFARIKI DUNIA KWENYE HELIKOPTA YA MMILIKI WA LEICESTER

  WATU watano wamefariki dunia pamoja na mmiliki wa klabu ya Leicester City ya England, bilionea Vichai Srivaddhanaprabha baada ya helikopta waliyokuwa wamepanda kuteketea kwa moto.
  Mmiliki wa Leicester City, Vichai Srivaddhanaprabha, mwenye umri wa miaka 60, ambaye aliinunua klabu hiyo kwa Pauni Milioni 39 mwaka 2010 na kuiwezesha kutwaa taji la ubingwa wa Ligi Kuu ya England mwaka 2016 atakumbukwa kama mtu wa kipekee na muungwana.
  Mlimbwende, Nursara Suknamai, Msaidizi wake, Kaveporn Punpare na rubani, Eric Swaffer, ambaye hapo kabla alisafirisha familia ya kifalme, na mpenzi wake na rubani mwenzake wake, Izabela Roza Lechowicz wote wamefariki kwenye ajali hiyo.

  Marubani Izabela Lechowicz na mpenzi wake, Eric Swaffer wakiwa kwenye helokpta kabla ya ajali 

  Inaaminika Rubani Swaffer aliokoa maisha ya mamia ya mashabiki kwa kuipeleka helikopta hiyo mbali na eneo la Uwanja iliporipuka.
  Helikopta hiyo iliteketea kwa moto baada ya kulipuka na kuungua nje ya Uwanja wa King Power mjini Leicester, Leicestershire juzi. 
  Tukio hilo lilitokea dakika chache tu baada ya mchezo wa Ligi Kuu ya England jana, Leicester City wakilazimishwa sare ya kufungana bao na 1-1 West Ham, wageni wakitangulia kwa bao la Fabian  Balbuena dakika ya 30 kabla ya Wilfred Ndidi kuwasawazishia wenyeji, dakika ya 89.
  Walioshuhudia tukio hilo wanasema kwamba waliona helikopta hiyo inaungua muda mfupi tu baada ya kuruka kutoka uwanjani hapo. 
  Kwa mujibu wa taarifa kutoka Leicester, Srivaddhanaprabha alikuwa anakwenda Uwanja wa Ndege wa Luton kupanda ndege ya kwenda Thailand. 
  Srivaddhanaprabha alikuwa mchora ramani wa taji la ubingwa wa Ligi Kuu ya England walilochukua Leicester katika msimu ambao walipanda kutoka Daraja la Kwanza, mwaka 2016.
  Aliibadilisha kabisa klabu hiyo baada ya kuinunua mwaka 2016 kwa dau la Pauni Milioni 39 mwaka 2010.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: WATANO WAFARIKI DUNIA KWENYE HELIKOPTA YA MMILIKI WA LEICESTER Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top