• HABARI MPYA

  Ijumaa, Oktoba 19, 2018

  RAIS DK MAGUFULI ALIPOKUTANA NA WACHEZAJI WA TAIFA STARS IKULU MJINI DAR ES SALAAM LEO

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na beki wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars', Kelvin Yondan  mara baada ya kuzungumza na kula nao chakula cha mchana Ikulu mjini Dar es Salaam leo
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Joseph Magufuli akimsabahi kipa wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars', Aishi Manula mara baada ya kuzungumza na kula nao chakula cha mchana Ikulu mjini Dar es Salaam leo 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akisalimiana na beki wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars', Erasto Nyoni mara baada ya kuzungumza na kula nao chakula cha mchana Ikulu mjini Dar es Salaam leo 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Joseph Magufuli akiwakabidhi Sh. Milioni 50, Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe pamoja na viongozi wa TFF ili zitumuke katika maandalizi ya mechi inayokuja ya kuwania kufuzi AFCON nchini Cameroon. Wengine katika picha ni Rais wa TFF Wallace Karia, Katibu Mkuu wa TFF Wilfred Kidao pamoja na Kaimu Nahodha wa Taifa Stars, Erasto Nyoni. 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Joseph Magufuli akijaribu jezi ya Taifa Stars aliyokabidhiwa na Kaimu Nahodha wa timu hiyo, Erasto Nyoni Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Joseph Magufuli akitoa maelekezo mara baada ya kukabidhi Sh. Milioni 50 kwa TFF kwa ajili ya maandalizi ya Taifa Stars Ikulu jijini Dar es Salaam leo 
  Beki wa Taifa Stars, Shomari Kapombe akijitambulisha mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam leo
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Joseph Magufuli akiwa katika chakula cha pamoja na  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe,Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Agustino Mahiga, Rais wa TFF Wallace Karia, Mwenyekiti wa Baraza la michezo (BMT) Rodger Tenga,Nahodha wa Timu ya Taifa Erasto Nyoni pamoja na wachezaji wengine wa Timu ya Taifa Stars.alipowaalika na kuzungumza nao Ikulu mjini Dar es Salaam.  
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Joseph Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Taifa Stars mara baada ya kuzungumza nao Ikulu mjini Dar es Salaam leo. Wengine katika picha mstari wa Mbele ni Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe watatu kutoka kushoto, Waziri wa Mambo ya Nje Balozi Dk. Augustine Mahiga watatu kutoka kulia akifatiwa na Injinia Leodgar Tenga, Mwenyekiti wa BMT, kocha wa timu ya Taifa Emanuel Amunike Pamoja na Katibu Mkuu wa TFF, Wilfred Kidao. Wengine ni Rais wa TFF Wallace Karia akiwa pamoja na Nahodha wa Timu ya Taifa Erasto Nyoni. 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Joseph Magufuli akizungumza na Wachezaji wa Taifa Stars 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: RAIS DK MAGUFULI ALIPOKUTANA NA WACHEZAJI WA TAIFA STARS IKULU MJINI DAR ES SALAAM LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top