• HABARI MPYA

  Jumanne, Oktoba 23, 2018

  MCHEZAJI CHIPUKIZI WA TANZANIA ALIYENG’ARA MICHUANO YA KUFUZU AFCON AENDA DENMARK KUFANYA MAJARIBIO

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MSHAMBULIAJI chipukizi wa Tanzania, Kelvin John ameondoka jana mjini Dar es Salaam kwenda Denmark kwa ajili ya majaribio ya kujiunga na klabu ya HB Koge inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza nchini humo.
  Kelvin amepata nafasi hiyo baada ya kufanya vizuri kwenye michuano maalum ya kuwania kushiriki Fainali za vijana chini ya umri wa miaka 17 Afrika (AFCON U17) kwa ukanda wa Afrika Mashariki, maarufu kama CECAFA AFCON Qualifier Tanzania ikimaliza nafasi ya tatu.
  Na akiwa Denmark, atapewa nafasi ya kufanya mazoezi na kucheza mechi za kirafiki na timu hiyo kwa 18, wastani wa wiki tatu huku makocha wa timu hiyo wakimfuatili.
  Kelvin John katika picha tofauti jana wakati wa safari yake 

  Kelvin John akiwa na tuzo yake ya Mchezaji Bora wa michuano ya kufuzu AFCON 

  Ikumbukwe Kelvin ni miongoni mwa vijana waliofanya vizuri kwenye mashindano ya CECAFA AFCON Qualifier yaliyofanyika mjini Dares Salaam Julai mwaka huu na ndiye mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa mashindano. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MCHEZAJI CHIPUKIZI WA TANZANIA ALIYENG’ARA MICHUANO YA KUFUZU AFCON AENDA DENMARK KUFANYA MAJARIBIO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top